Maelfu ya watu wameuawa nchini Sudan tangu vita kati ya vikosi hasimu vilipozuka katikati ya Aprili 2023. / Picha: Reuters

Jeshi la Sudan lilisema siku ya Jumamosi lilizima shambulio "kubwa" lililofanywa na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) katika mji wa El Fasher, katikati mwa jimbo la Darfur Kaskazini magharibi mwa nchi.

Jeshi lilisema kuwa vikosi vyake vilizima shambulio hilo kubwa na kusababisha hasara kubwa.

Vuguvugu la Ukombozi wa Sudan, ambalo lilipigana pamoja na jeshi, pia lilisema RSF ilijaribu "kuikalia" El Fasher kwa kushambulia kutoka pande zote - kaskazini, kusini, magharibi na mashariki - na maelfu ya wanamgambo.

Vita nchini Sudan vilizuka mwezi Aprili 2023 kati ya Jenerali wa Jeshi Abdel Fattah al-Burhan na kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo kwa sababu ya kutofautiana kuhusu kuijumuisha RSF katika jeshi.

TRT Afrika