Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) limekanusha madai kuwa walinda amani wake walihusika na vitendo vya unyanyasaji wa kingono.
RDF, ambayo ilikuwa ikijibu tuhumu hizo zilizochapishwa kama makala kwenye moja ya vyombo vya habari kuwa wanajeshi wake walihusika na tuhumu za ubakaji Jamhuri ya Afrika ya Kati.
“Katika tuhuma ya kubakwa binti aitwaye Grace katika mji wa Paoua, tungependa kusisitiza kuwa hakuna mlinda usalama wa Rwanda aliyetumwa kufanya kazi katika eneo hilo, kwahiyo tuhuma hizo hazina msingi wowote,” ilisema taarifa ya RDF.
Katika tuhuma nyingine ya ubakaji kwenye eneo la Ndassima, lililo kilomita 400 kutoka Bangui, RDF iliweka bayana kuwa majeshi ya Rwanda MINUSCA hayakutumwa kufanya kazi katika eneo hilo.
Taarifa hiyo iliongeza: Jeshi letu haliruhusu vitendo vyovyote vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya raia.
Hali kadhalika, RDF ilisisitiza kuwa itaendelea kuunga mkono shughuli za kulinda amani Jamhuri ya Afrika ya Kati na kokote pale jeshi hilo litakapotumwa.