Mnamo 2017, Nandi-Ndaitwah alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa chama tawala cha SWAPO, mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi hiyo / Picha: AFP

Ndemupelila Netumbo Nandi-Ndaitwah aliyezaliwa Oktoba 29, 1952 ni mwanasiasa wa Namibia anayehudumu kama Makamu wa Rais wa Namibia tangu Februari 2024.

Pia ni mgombea urais wa kwanza mwanamke wa SWAPO katika uchaguzi mkuu wa 2024 wa Namibia.

Mnamo 2017, Nandi-Ndaitwah alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa chama tawala cha SWAPO, mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi hiyo.

Safari ya siasa

Nandi-Ndaitwah hapo awali aliwahi kuwa naibu waziri mkuu wa Namibia kuanzia 2015 hadi 2024, waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia Disemba 2012 hadi 2015, na kama waziri wa Mazingira na Utalii kuanzia Machi 2010 hadi Disemba 2012.

Yeye ni mwanachama wa muda mrefu wa Bunge.

Amekuwa mjumbe wa Bunge la Namibia tangu 1990.

Kufuatia kifo cha Rais Hage Geingob wa Namibia mnamo Februari 2024, Nandi-Ndaitwah aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais, akimrithi Nangolo Mbumba ambaye aliteuliwa kuwa rais wa mpito/ Picha Reuters 

Alikuwa naibu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano kutoka 1990 hadi 1996 na alipata hadhi ya uwaziri mnamo 1996 kama mkurugenzi mkuu wa Masuala ya Wanawake katika Ofisi ya Rais. alihudumu hadi 2000.

Mnamo 2000 alipandishwa cheo na kuwa waziri na kupewa wadhifa wa Masuala ya Wanawake na Ustawi wa Watoto.

Kuanzia 2005 hadi 2010, alikuwa Waziri wa Habari na Utangazaji katika baraza la mawaziri la Namibia.

Chini ya Rais aliyefariki Hage Geingob, Nandi-Ndaitwah aliteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Namibia Machi 2015 / Picha: photo Nandi-Ndaitwah  kwa X

Baadaye alihudumu kama Waziri wa Mazingira na Utalii hadi mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri mnamo Desemba 2012, ambapo aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, wizara ambayo tangu ilipobadilishwa jina na kuwa Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano.

Chini ya Rais aliyeaga Hage Geingob, Nandi-Ndaitwah aliteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Namibia Machi 2015, huku akihudumu sambamba na kuwa Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano.

Mnamo Machi 2023, Rais Geingob alimtaja Netumbo Nandi-Ndaitwah kama mgombea urais wa SWAPO katika uchaguzi mkuu wa Namibia wa 2024.

Kufuatia kifo cha Geingob mnamo Februari 2024, Nandi-Ndaitwah aliteuliwa kuwa makamu wa rais, akimrithi Nangolo Mbumba ambaye aliteuliwa kuwa rais wa mpito hadi uchaguzi mkuu wa Novemba 2024.

Yeye ndiye mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi hiyo.

TRT Afrika