Nchi nne katika kanda ya Afrika Mashariki zimesoma bajeti zao zikizngazia kuinua uchumi zao / Picha : AFP / Photo: AP

Na Coletta Wanjohi

Nchi mbalimbali za Afrika mashariki hii leo zimesoma bajeti za mwaka wa fedha 2023 kwa 2024. Mambo mbalimbali yameainishwa katika bajeti hizo.

Tanzania

Katika bajeti yake, Tanzania imezingatia kuwekeza zaidi katika gesi asilia, ujenzi wa barabara na madaraja, na kuendeleza maeneo maalum mkiwemo uwekezaji Bagamoyo.

Kipaumbele pia kimepewa kwa Ujenzi wa reli ya standard gauge (SGR), kukarabati Kampuni ya Air Tanzania (ATCL), ujenzi wa mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (MW 2,115) na ujenzi wa miradi ya nishati ya Ruhudji (358 MW) na Rumakali (MW 222).

Waziri wa Fedha, Dkt, Mwigulu Nchemba amesema serikali pia imekamilisha taratibu zitakazoiwezesha Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kununua dhahabu, huku nchi ikilenga kuongeza akiba, na kutengeza bei na sarafu yake,

Serikali pia imekamilisha taratibu zitakazo iwezesha Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kununua dhahabu, huku nchi ikilenga kuongeza akiba. Picha Wizara ya Fedha Tanzania

“Fedha zitawekwa na Serikali kurejesha mtaji kwa benki zake ikiwemo, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Benki ya Maendeleo TIB na Benki ya Biashara Tanzania (TCB). na shilingi bilioni za Tanzania 235.9 baada ya kutathmini hali ya benki hizo," Nchemba amesema.

Serikali pia imetetea biashara binafsi.

" Serikali inapendekeza kuanzia Julai 1, mwaka huu, ni marufuku kwa mamlaka yoyote ya udhibiti kufunga shughuli za biashara kutokana na kukiuka sheria mbalimbali."

Uganda

Nchini Uganda serikali imeipa kipaumbele sekta ya kilimo,kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, kupigana na athari za tabianchi na kuboresha mazao.

Fedha pia zimetengwa kwa ajili ya kuinua biashara binafsi, serikali ikiangazia utalii, maendeleo ya viwanda na uvumbuzi.Uganda. Picha Wizara ya fedha Uganda

"Ni lazima kila juhudi ifanyike kuongeza thamani ya bidhaa zetu zote, kuongeza thamani ya kahawa, tutapata pesa mara kumi zaidi ya tunayouza sasa, pamba, mbao, kakao, mazao ya samaki, dhahabu, chuma, shaba, mbolea, " rais wa Uganda Yoweri Museveni ameiambia bunge la Uganda .

Fedha pia zimetengwa kwa ajili ya kuinua biashara binafsi, serikali ikiangazia utalii, maendeleo ya viwanda na uvumbuzi.

Katika hali ya kuangalia maisha ya wananchi serikali imeangazia rasili mali zaidi katika afya, elimu na huduma ya maji.

Kenya

Waziri wa fedha wa Kenya, Njunguna Ndung'u awasilisha bajeti bungeni / Picha : AFP

Kenya imependekeza kuongeza kiwango cha ushuru wa bidhaa kwenye kamari, michezo ya kubahatisha, mashindano ya bei na bahati nasibu kutoka asilimia 7, ya sasa hadi 12. Utumaji wa ushuru wa bidhaa utafanywa ndani ya masaa 24 baada ya kufungwa kwa muamala.

Bunge la Kitaifa limependekeza kupunguzwa kwa ushuru wa asilimia15 ya michango kwa hazina yawafanyikazi kwa ajili ya matibabu ya watu baada ya kustaafu au kuwapatia dola 35 kwa mwezi. Hii ina nia ya kuhimiza wafanyikazi kuweka akiba kwa mahitaji yao ya baada ya kustaafu.

Bidhaa za petroli mafuta ya petroli zitatozwa ushuru wa asilimia 16%.

Ili kuhimiza uongezaji wa thamani wa mazao ya chai imependekezwa kuondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye chai iliyonunuliwa viwandani au katika vituo vya mnada vya chai kwa ajili ya kuongeza thamani na kuuza nje ya nchi.

Serikali imependekeza Ushuru wa Bidhaa kwenye sukari inayoagizwa kutoka nje. Lakini hii haijumuishi sukari inayoagizwa kutoka nje au kununuliwa nchini na watengenezaji wa dawa waliosajiliwa.

Serikali inasema hii ni kwa nia ya kupunguza unywaji wa sukari ambao umekuwa ukihusishwa na magonjwa mbalimbali.

Serikali pia imependekeza fedha kwa ajili ya miradi ya serikali ya kuimarisha uzuiaji na kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia nchini Kenya.

Rwanda

Katika bajeti yake ya taifa,serikali ya Rwanda ilisema kupanda kwa matumizi kutachochea ufufuaji wa uchumi .

Kipaumbele kiliwekwa katika uwekezaji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na pia kufadhili uwekezaji muhimu katika elimu, huduma za afya, teknolojia na uvumbuzi na miundombinu kupitia mkakati wa kitaifa ambao umewekwa tayari.

Serikali ya Rwanda ilisema kupanda kwa matumizi kutachochea ufufuaji wa uchumi . Picha Wizara ya Fedha Rwanda

TRT Afrika