Human Rights Watch inadai Israel imetumia kemikali ya fosforasi nyeupe katika mashabulizi Gaza na Lebanon  / Picha: AA

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limesema Israel imetumia kemikali ya fosforasi nyeupe ( White phoshorus ) katika operesheni zake za kijeshi Lebanon na Gaza.

Fosforasi nyeupe huchoma sana na inaweza hata kuwasha nyumba moto.

Matumizi yake katika maeneo yenye watu wengi ni kinyume cha sheria.

" Kulingana na akaunti za video zilizothibitishwa na mashahidi kwamba vikosi vya Israeli vilitumia fosforasi nyeupe katika operesheni za kijeshi huko Lebanon na Gaza mnamo Oktoba 10 na 11, 2023, mtawalia," Shirka hilo limesema katika mtandao wake wa X.

Human Rights Watch inasema huu "ni ushahidi wa uhalifu wa kivita" kwani ina uwezo wa kuleta hatari ya majeraha makubwa na ya muda mrefu.

Fosforasi Nyeupe ( White phoshorus ) ni ni hasa?

Fosforasi nyeupe ni kemikali ambayo hutawanywa katika makombora ya mizinga, mabomu na roketi, ambayo huwaka inapofunuliwa na oksijeni au hewa safi.

Watu wengi wameuawa na wengine kujeruhiwa katika vita kati ya Israel na wapiganaji wa Hamas ulianza 7 Oktoba mwaka huu. picha: Reuters 

Kemikali hii hutoa joto kali la nyuzi joto 815.

Hutoa mwanga na moshi mzito unaotumiwa kwa madhumuni ya kijeshi, lakini pia husababisha majeraha ya kutisha wakati fosforasi inapogusana na watu.

Haichukuliwi kama silaha ya kemikali kwa sababu inafanya kazi hasa kwa kutumia joto badala ya sumu.

Fosforasi nyeupe inatumika vipi?

Fosforasi nyeupe hutumiwa kimsingi kuficha shughuli za kijeshi ardhini.

Inaweza kuunda wingu la moshi usiku au wakati wa mchana ili kuficha harakati za kuwaona wanajeshi. Pia huingilia mifumo ya macho na ufuatiliaji wa silaha, hivyo basi kulinda vikosi vya kijeshi dhidi ya silaha zinazoongozwa kama vile makombora ya kukinga vifaru.

Athari zake kwa binadamu

Fosforasi nyeupe husababisha kuchomeka kali, mara nyingi chini ya mfupa, ambayo inachukua muda sana kupona na muathirika anaweza kupata maambukizi.

Fosforasi nyeupe ilitumiwa katika vita vya zamani, ikiwa ni pamoja na vita vya Kwanza na vya pili vya Dunia  / Picha: AA

Ikiwa vipande vyote vya fosforasi nyeupe havijaondolewa, vinaweza kuimarisha majeraha baada ya matibabu na kuleta mathara kila mara ikipatana na oksijeni.

Fosforasi nyeupe ikichoma asili mia 10 tu ya mili wa mtu ni hatari sana na mara nyingi husababisha kifo.

Inaweza pia kusababisha uharibifu wa kupumua na kushindwa kwa viongo vyamwili kufanya kazi.

Wale wanaonusurika majeraha yao ya awali mara nyingi huishi kwa mateso na uchungu maishani.

TRT Afrika