Iran yapongeza nchi za Kiafrika kwa upinzani wake dhidi ya 'ukoloni'

Iran yapongeza nchi za Kiafrika kwa upinzani wake dhidi ya 'ukoloni'

Iran yapongeza nchi za Kiafrika kwa upinzani wake dhidi ya 'ukoloni'
Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso, Olivia Rouamba, akiwa ziara yake nchini Iran/ Picha: AFP

Rais wa Iran Ebrahim Raisi amezipongeza nchi za Afrika kwa kupinga "ukoloni" baada ya kumpokea waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Olivia Rouamba.

Burkina Faso na Mali, zinaongozwa na watawala wa kijeshi ambao walikata uhusiano wa kijeshi na Ufaransa, nchi ambayo ilikuwa ya kikoloni, na kuimarisha uhusiano wake na Urusi.

Aidha, Niger, ambako hivi majuzi, wakuu wa kijeshi walichukua mamlaka mwezi Julai, lilishuhudia maandamano makubwa ya raia huku wakitaka wanajeshi wa mtawala wa zamani wa kikoloni, Ufaransa kuondoka.

Siku ya Jumatatu, rais wa Iran Raisi, bila kuitaja Ufaransa, "alisifu upinzani wa nchi za Kiafrika kupinga ukoloni na ugaidi" wakati wa mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso Olivia Rouamba.

Wakati huo huo, alisifu msimamo wa Afrika kama "ishara ya kuwa macho na mwamko," kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya rais wa Irani.

Burkina Faso ilishuhudia mapinduzi ya kijeshi mara mbili ndani ya mwaka wa 2022, na utawala wa kijeshi baadaye ukataka wanajeshi wa Ufaransa kuondoka nchini humo.

Kwenye mkutano na Waziri Rouamba, Raisi alieleza nia ya Iran "kugawa uzoefu na mafanikio yake na nchi rafiki za kiafrika."

Kwa upande mwingine, Rouamba pia alionyesha nia ya kuimarisha uhusiano wa pande mbili na Iran, kulingana na taarifa kutoka Ikulu ya Irani.

Iran imekuwa ikiimarisha uhusiano wake katika bara la Afrika kama juhudi za kupunguza kutengwa kwake na kutatua athari za vikwazo vilivyowekwa kwake tena tangu Merekani kujiondoa kutoka kwa makubaliano ya nyuklia yaliyojadiliwa kwa uchungu mnamo 2018.

Mnamo mwezi Julai, rais wa Iran Raisi alianza ziara adimu ya Afrika na kusafiri hadi Kenya, Uganda na Zimbabwe.

AFP