Taarifa zinaonyesha Malawi imepata ndege hizo kati ya mwaka 1986 na 1989/ Picha: wengine 

Ndege iliyosababisha kifo cha Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima na abiria wengine tisa Juni 10 imefahamika kama Donier 228-202K.

Ajali hiyo ilitokea katika Msitu wa Chikangawa kaskazini mwa Malawi, muda mfupi tu baada ya ndege hiyo kupata mawasiliano ya kurudi mji mkuu wa Lilongwe kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa mzuzu.

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amesema ndege hiyo imeshindwa kutua katika uwanja wa ndege wa mzuzu kutokana na hali mbaya ya hewa.Wataalamu wa masuala ya anga Cirium wanasema jeshi la Malawi limekuwa likitumia ndege tatu za Dornier.

Taarifa zinaonyesha Malawi imepata ndege hizo kati ya mwaka 1986 na 1989.

Dornier imetengenezwa na kampuni ya Ujerumani ambayo ilisitisha uzalishaji mwaka 2002 kutokana na matatizo ya kifedha. Kampuni hiyo iliasisiwa na mhandisi wa kijerumani Claudius Dornier mwaka 1914.

Ndege ya 228-202K ina uwezo wa kubeba abiria 18 na marubani wawili. Picha: Wengine 

Wakati ilipofungwa, Dornier alikuwa ameuza zaidi ya ndege 1,000 duniani kote.

Ndege ya 228-202K ina uwezo wa kubeba abiria 18 na marubani wawili.Ina uwezo wa kubeba uzito wa kilo 6,200, na inaweza kukimbia kilomita 430 kwa saa. Uwezo wake wa kuruka ni juu ya usawa wa bahari ni futi 25,000.

Toleo la Dornier 228 lina ingini mbili ambazo zinasukuma mabawa.Toleo la mwaka 1989 linagharimu kiasi cha dola milioni 2.3.

Hivi sasa, taarifa zinaonyesha kuwa takriban matukio 96 ya angani yamehusishwa na ndege hiyo.Jumla ya vifo 218 vimetokea katika maeneo tofauti ya dunia.Toleo hasa, – Dornier 228-202K – limesababisha vifo 12 kati yam waka 2008 na 2024, huku vifo kumi vikiwa ni vile vilivyotokea Juni 10 nchini Malawi.

Taarifa kutoka Mtandao wa Anga Salama unaonyesha vifo vyengine viwili vilitokea Chile September 2013.Mbali na ajali zilizosababisha vifo, ndege hiyo aina ya 228-202K pia imehusika katika ajali katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ufilipino, Nepal, Australia na India.

Toleo la kubwa la Dornier 228, hata hivyo limerekodi vifo kadhaa.Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa mfano, ndege ya kibiashara ya Dornier 228-201 ilipata ajali na kusababisha vifo vya watu 27 katika mji wa mashariki mwa Goma November 24, 2019.

Nchini Nigeria, ndege ya Dornier 228-212 iliyokuwa inatumiwa na jeshi la nchi hiyo, ilipata ajali na kuuwa watu 13 katika Jimbo la Benue September 2006.

Kwa mara nyengine, Nigeria, tukio linalofanana la ndege ya Dornier inayomilikiwa na jeshi la anga, ilianguka katika eneo la makazi ya watu katika jimbo la kaskazini la Kaduna mwezi Agosti 2015, na kusababisha vifo vya watu saba.

Ajali nyengine mbaya zaidi ilihusisha ndege ya Dornier ilitokea Cape Verde katika Agosti 1999, pindi ajali hiyo iliposababisha vifo vya watu 18.

Nchini Sudan ya Kusini katika mji wa Pibor, mtu mmoja alipoteza maisha Septemba 2020. Kati yam waka 1992 na 2024, Nigeria imepata ajali 3 ya ndege ya Dornier bila kusababisha vifo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imekuwa na ajali mbili, Sao Tome na Principe 1, na Somalia 1.

Nje ya Africa, ajali ya ndege ya Dornier imesababisha vifo vya watu 11 magharibi mwa India mwaka 1989, na watu 19 Nepal 1993.

Bado huko huko Nepal, watu 14 walipoteza maisha mwaka 2010, na wengine 15 mwaka 2012.

TRT Afrika