Jeshi, ambalo hivi karibuni limeripoti mafanikio dhidi ya RSF katika sehemu za mji mkuu, lilisema Keikal ameamua kuchukua hatua hiyo kwa sababu ya "ajenda ya uharibifu" ya RSF/ Picha : Reuters

Idadi ya watu waliouawa na wapiganaji kutoka kikosi cha dharura cha RSF nchini Sudan, imeongezeka kufikia watu 124 katika kijiji kimoja katika Jimbo la El Gezira siku ya Ijumaa, wanaharakati walisema, katika moja ya matukio mabaya zaidi ya vita vya miezi 18 na kubwa zaidi katika mfululizo wa mashambulizi katika jimbo hilo.

Kufuatia kujisalimisha kwa afisa wa ngazi ya juu wa RSF Abuagla Keikal kwa jeshi Jumapili iliyopita, wanaharakati wanaounga mkono demokrasia walisema RSF imefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi katika jimbo la kilimo anakotoka, na kuua na kuwaweka kizuizini raia na maelfu ya watu kuyahama makazi yao.

Gezira tayari amekabiliwa na msukosuko wa miezi kadhaa ambapo wakaazi waliiambia Reuters kuwa RSF walipora nyumba, kuua raia wengi na kuwakimbia mamia kwa maelfu.

Kijiji cha Al-Sireha, kaskazini mwa jimbo hilo, kilikumbwa na ghasia mbaya zaidi za hivi majuzi ambapo takriban 124 waliuawa na 100 kujeruhiwa katika uvamizi wa RSF, Kamati ya Upinzani ya Wad Madani, kundi linalounga mkono demokrasia, lilisema Jumamosi.

RSF yadai Keikal 'alipewa dili'

Katika taarifa siku ya Ijumaa, RSF ilishutumu jeshi kwa kuwapa silaha raia huko Gezira na kutumia vikosi chini ya amri ya Keikal, na kusababisha mashambulizi yake.

Wiki iliyopita, Wafuasi wa jeshi walichapisha picha mtandaoni zinazodai kumuonyesha Abuagla Keikal - afisa wa zamani wa jeshi ambaye alikua kamanda mkuu wa RSF katika jimbo la kusini mashariki la El Gezira - baada ya kuhama.

Baadaye RSF ilichapisha taarifa ikidai kuwa Keikal alibadili upande wake baada ya "dili", na kusema kuwa imesababisha hasara kwa vikosi vilivyoasi mashariki mwa jimbo la El Gezira, ambako Keikal anatoka.

Jeshi, ambalo hivi karibuni limeripoti mafanikio dhidi ya RSF katika sehemu za mji mkuu, lilisema Keikal ameamua kuchukua hatua hiyo kwa sababu ya "ajenda ya uharibifu" ya RSF.

Hakukuwa na maoni ya mara moja kutoka kwa Keikal, ambaye alikuwa afisa wa ujasusi wa kijeshi kabla ya vita.

Vita hivi vinavyoongozwa zaidi na Jeshi la taifa na wapiganaji wa RSF, limeendelea kwa miezi 18 bila dalili za mafanikio huku maelfu ya raia wakiuawa, mamilioni kukimbia na wengi kuejruhiwa.

Reuters