Rais Ghazouani anawania kuchaguliwa tena/ Picha: Reuters

Rais wa Mauritania anayemaliza muda wake, Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani amesema atakahakikisha kuwa zoezi la uchaguzi la nchini humo linakuwa la huru na haki, huku wapinzani wakiibua madai ya udanganyifu katika mchakato huo.

Alisisitiza nia ya kuheshimu matokeo ya uchaguzi huo.

Wakati huo huo, mgombea kutoka kambi ya upinzani Biram Dah Abeid ameituhumu Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kwa kupanga njama za kulaghai wakati wa uchaguzi huo.

Baada ya kupiga kura yake katika kituo kilichopo mjini Nouakchott, Ghazouani alisema kuwa tume hiyo "ilisambaza karatasi za kupigia kura kwa wafuasi wa mgombea kutoka chama tawala," huku tume hiyo ikishindwa kutoa majibu yoyote kufuatia tuhuma hizo.

'Uwezekano wa Udanganyifu'

Kiongozi wa upinzani na mkuu wa chama cha National Rally for Reform and Development, Hamadi Ould Sid' El Moctar, amesema yuko tayari kukubaliana na matokeo iwpo tu "uchaguzi huo utakuwa ni wa haki na uwazi," huku akionya dhidi ya "udanganyifu wowote unaoweza kutokea."

Alisisitiza umuhimu wa kudumisha usalama wakati wa uchaguzi, akibainisha kuwa dalili zote zinaonesha kuwa "wananchi wanataka mabadiliko."

Siku ya jumamosi asubuhi, Wamauritania walianza kupiga kura kuchagua rais mpya kati ya wagombea saba, akiwemo Rais aliye madarakani Ghazouani.

Iwapo hakuna atakayepata wingi wa kura, basi wagombea wawili wa juu watashiriki duru ya pili Julai 13.

TRT Afrika