Gbagbo aliachiwa huru na ICC mwaka 2019. Picha: AFP  

Kiongozi wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo amekubali kugombea tena Urais pamoja na kuwa alipoteza sifa hiyo baada ya hukumu yake ya miaka 20 jela, chama chake kimesema.

Laurent Gbagbo alikuwa Rais wa kwanza wa zamani kushtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu(ICC) mjini The Hague na kisha kuachiwa huru mwaka 2019.

Amekubali kuwa mgombea wa chama cha PPA-CI" (African People's Party-Ivory Coast) kufuatia kikao cha halmashauri kuu ya chama," ilisema taarifa iliyotolewa Jumapili.

Pamoja na kuondolewa mashtaka yake ya uhalifu dhidi ya ubinadamu mjini The Hague, Gbagbo alihukumiwa miaka 20 jela kwa kosa la kufanya uhalifu benki.

Kipaumbele kikuu

Gbagbo alipoteza uchaguzi wa mwaka 2010 baada ya kushindwa na Ouattara, lakini aligoma kuachia madaraka, kitendo kilichoamsha umwagaji mkubwa wa damu, hali iliyopelekea majeshi ya Ufaransa na yale Umoja wa Mataifa kuingilia kati.

Mwaka 2022, alipata msamaha wa Urais kutoka kwa kiongozi wa sasa na hasimu wake wa siku nyingi Ouattara na kukosa sida za kugombea Urais mwakani.

Chama chake kimeweka wazi kuwa kitaitisha mkutano ili kumuidhinisha Gbagbo kama mgombea katika uchaguzi huo, ambacho ni kipaumbele cha chama hicho.

Chama hicho kikaongeza kuwa kitaweka jina la Gbagbo kwenye orodha ya wagombea.

Wagombea wengine

Hukumu yake ya 2018 ilimuondolea mwanasiasa huyo haki yake ya kugombea uongozi.

Disemba mwaka jana, chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Democratic Party of Ivory Coast (PDCI)kilimteua Tidjane Thiam kama Rais wake mpya.

Hata hivyo, si Thiam wala Alassane Ouattara walioonesha nia ya kugombea kwenye uchaguzi wa Rais mwaka 2025.

TRT Afrika