Automjeti i ambasadorit turk në Sudan goditet me armë zjarri / Photo: Reuters

Gari rasmi la balozi wa Uturuki nchini Sudan lilipigwa risasi siku ya Jumamosi, wakati mapigano yakiendelea kati ya jeshi na kundi la wanamgambo katika mji mkuu Khartoum na mazingira yake.

Hakuna hasara iliyoripotiwa na chanzo cha milio ya risasi iliyolipiga gari la Ismail Cobanoglu hakijafahamika, zilisema duru za kidiplomasia za Uturuki, zikizungumza kwa sharti la kutotajwa majina kwani hawakuwa na idhini ya kuzungumza na vyombo vya habari.

Mapigano kati ya majenerali wawili hasimu - mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na kamanda wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) Mohammed Hamdan "Hemedti" Dagalo - yalizuka Aprili 15, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 550 na maelfu kujeruhiwa hadi sasa.

Kutokubaliana kumekuwa kukizuka katika miezi ya hivi karibuni kati ya pande hizo mbili kuhusu kuunganishwa kwa RSF katika jeshi - sharti linalotajwa kuwa muhimu la makubaliano ya mpito ya Sudan na makundi ya kisiasa.

Sudan imekuwa bila serikali ya kiraia inayofanya kazi tangu mwaka 2021 wakati jeshi lilipofuta serikali ya mpito ya Waziri Mkuu Abdalla Hamdok na kutangaza hali ya hatari katika hatua iliyotajwa na vikosi vya kisiasa kama "mapinduzi."

Kipindi cha mpito, kilichoanza Agosti 2019 baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais Omar al-Bashir,awali kilipangwa kumalizika na uchaguzi mapema 2024.

AA