Nyufa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) zinaonekana kupanuka tangu mabadiliko ya serikali nchini Niger Julai 26 mwaka jana, na kulazimisha Umoja wa Kikanda kuwa katika hali ya kutatua matatizo yaliyopo.
Mpango wa kutatua hali hio uzio unakuja baada ya kupungua kwa taratibu wuungwaji mkono kwa jumuiya hio, baada ya serikali ya kijeshi nchini Niger ikiungana na wenzao wa Mali na Burkina Faso kuunda Shirikisho la des États du Sahel, au Muungano wa Nchi za Sahel (AES).
ECOWAS imekuwa ikichukua hatua za hatari kwa zaidi ya mwaka mmoja, na uamuzi wake wa kukata usambazaji wa umeme na kufunga mipaka ya nchi ya Niger isiyokuwa na bandari, ilishajiisha azima ya nchi hio kuondoka kwenye jumuia hio pamoja na nchi zingine mbili zinazotawaliwa na kijeshi za Afrika Magharibi.
Kuanzishwa kwa kikosi cha kijeshi na kuwekwa tayari kwa ajili ya uingiliaji kati unaowezekana kurejesha demokrasia nchini Niger kulionekana kuwa ni hatua ya mwisho ya kuvuruga uhusiano.
Burkina Faso na Mali, ambazo zilishuhudia mapinduzi mwaka 2021 na 2022, zilikubaliana na Niger kwamba zilihitaji kujitenga na ECOWAS ili kuunda kambi tofauti kama ngome dhidi ya uvamizi wa ndani na nje.
Ingawa ECOWAS iliondoa vikwazo hivyo katika hatua ya maridhiano baadaye, lakini baada ya kuvuruga uhusiano.
Jumuiya ya AES sasa ni changamoto ya kweli ambayo inahitaji kushughulikiwa.
Misheni ya upatanisho
Tangu kuchaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa ECOWAS, Rais Bola Ahmed Tinubu wa Nigeria amekuwa akijitahidi kurejesha ufanisi wa juimuiya hio.
ECOWAS imewapa Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye na mwenzake wa Togo Faure Gnassingbé kazi ngumu ya kuzishawishi Mali, Niger na Burkina Faso kurudi kwenye jumuiya.
Faye, ambaye alipata kazi hiyo katika mkutano wake wa kwanza wa ECOWAS, ni miongoni mwa viongozi vijana zaidi wa eneo hilo na anaonekana kuwa mtu anayeweza kuleta mtazamo mpya mezani.
"Kama mwenyekiti wa ECOWAS, ninakualika ushirikiane na kukutana na ndugu wengine ili kuwashawishi kurejea kundini," Tinubu alimwambia Faye katika mkutano mjini Abuja.
Tangu yeye na Gnassingbé walichaguliwa kuanzisha upatanisho, Faye tayari ametembelea Mali na Burkina Faso kujaribu kufanikisha misheni hiyo.
Sababu za mafanikio
Huku tarehe ya mwisho ya Januari 2025 iliyowekwa kwa mataifa matatu yaliyojitenga kujiunga tena na jumuiya ya kikanda inakaribia, watu wamekuwa wakiangalia mambo yanayoweza kusaidia mafanikio ya mpango huo ili kuwashawishi na kwamba kurejea katika jumuiya ya ECOWAS ni kwa manufaa ya kila mtu.
Wachambuzi wanaamini kwamba moja ya mambo ambayo yanaweza kufanya kazi katika kufanikisha maridhiano ni kutumia uafrika na fikra ya dhidi ya wabeberu ambayo Faye na mmoja wa washauri wake, Ousman Sonko, walitumia katika kampeni ya kura ya urais wa Senegal mwaka huu.
"Uhusiano wa kiitikadi upo, na ni muhimu sana kutumika katika mazingira kama hayo," Prof Aliou Sow, waziri wa zamani wa Senegal, anaiambia TRT Afrika.
Sababu nyingine muhimu ya kuaminiana ni kwamba asilimia kubwa ya biashara iliyoko kati ya Mali na Senegal.
"Ahadi ya Senegal ya kuunga mkono kijeshi Mali katika mapambano yake dhidi ya makundi ya kigaidi, kama ilivyotangazwa na (Waziri Mkuu) Ousmane Sonko inapaswa kuwa muhimu katika misheni ya upatanisho," anaeleza Prof Sow.
"Jambo muhimu ni kwamba wanahitaji kuwa na ECOWAS kuelewa muktadha wa maamuzi kama haya yanayohusisha nchi hizo mbili."
Kitu kingine ambacho kinaelekea kwenda vyema kwa misheni ya upatanisho ni utaalamu wa mpatanishi mwenzake wa Faye, Gnassingbé.
Uhusiano wa kiongozi huyo na baadhi ya viongozi wa nchi za AES na uzoefu wake katika kutatua mizozo unaonekana kuwa wa thamani sana katika hali ya sasa.
"Ingawa bado ni kijana, anaonekana kama kiongozi mkuu wa eneo ambaye anakuza uhusiano wa amani," anasema Prof Sow.
Vizuizi vinavyoweza kujitokeza
Kwa mujibu wa Issoufou Boubacar Kado Magagi, mchambuzi aliyeko Niamey, mojawapo ya changamoto ni dhana miongoni mwa baadhi ya watu kwamba jumuiya ya kikanda inaegemea upande wa madola ya Magharibi, hususan Ufaransa.
Magagi anasema kuwa wajumbe kadhaa wa nchi za Magharibi walihudhuria mkutano wa mwisho wa ECOWAS, na kupendekeza wana jukumu la kutekeleza katika msimamo wa jumuiya hiyo.
"Nyakati zimebadilika. Katika nchi za Afrika, vijana hawakubali vita hivi vya uasi ambavyo vinatumia baadhi ya viongozi wa Afrika kusukuma ajenda ya Magharibi," Magagi anaiambia TRT Afrika.
Wachambuzi kama yeye pia wanaamini kuwa dhamira ya ECOWAS itakuwa na matokeo chanya zaidi kwa kutoa fidia kwa biashara ambazo zilipata hasara kutokana na vikwazo vilivyowekwa na jumuiya hiyo.
"Mipaka ilipofungwa, tulikuwa na bidhaa nyingi zilizokwama katika bandari ya Cotonou. Biashara zilipoteza mamilioni ya faranga za CFA. Hakuna anayezungumza kuhusu kuzifidia," anasema Magagi.
Dawa ya mafanikio
Licha ya vikwazo vilivyopo mbele ya wakuu hao wawili wa nchi wanaoongoza ujumbe wa maridhiano, kuna matumaini kwamba wawili hao wanaweza kuzuia kuondoka kabisa kwa nchi za AES kutoka ECOWAS kwa hatua fulani.
Kulingana na wachambuzi, moja ya hatua hizo ni kuendelea kupunguza shinikizo na mazungumzo makali na badala yake kufanya majadiliano na makubaliano ambayo yangefaidi pande zote mbili.
"Nafikiri kwamba Faye anaweza kubuni mkakati wa kidiplomasia wenye pande mbili - yeye ashughulike na viongozi wa ECOWAS na Waziri Mkuu wake (Ousmane Sonko) na viongozi wa junta," Prof Sow anaiambia TRT Afrika.
Ziara ya Agosti 12 ya Sonko nchini Mali inaonekana kama hatua katika mwelekeo huu.
Baadhi ya wachambuzi wanaamini kuwa ziara za wawakilishi wa nchi zenye muono wa pamoja dhidi ya utawala wa Magharibi, hasa ule wa mataifa yenye nguvu za kikoloni kama vile Ufaransa, ni sehemu muhimu ya jitihada za kurudisha uhusiano kati ya nchi hizo tatu na ECOWAS.