Msanii wa Nigeria Oluwatobiloba Fasalejo anatumia sanaa yake ya uchoraji katika kufikisha ujumbe. Picha: Fasalejo  

Na Pauline Odhiambo

Katika lugha ya Kiyoruba, neno Fasalejo lina maanisha mtu mwenye kujali na mkarimu. Tafsiri hii inaakisi sifa za Oluwatobiloba Fasalejo, mchoraji kutoka Nigerai anayetumia sanaa yake katika kufikisha ujumbe kwa jamii yake.

“Tayari tulikuwa na vitu vingi vibaya vinatokea nchini Nigeria na ulimwenguni kwa ujumla, na ndio maana nimetumia michoro yangu kuwapa watu tulizo,” anasema mchoraji huyo katika mahojiano yake na TRT Afrika.

“Kiu yangu ni kuona watu wakijitazama kupitia kazi zangu.”

Kulingana na jarida la Artland, sanaa ya kujieleza ni mtindo wa kisanii ambamo msanii hutafuta kuonysha ukweli usio halisi, lakini hisia na majibu ya kibinafsi.

Sanaa ya kujieleza ni mtindo wa kisanii ambamo msanii hutafuta kuonysha ukweli usio halisi, lakini hisia na majibu ya kibinafsi./Picha: Fasalejo

Sanaa yenye akili

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Jimbo la Ondo, daima amekuwa akiwakumbuka wengine.

Toka akiwa mtoto mdogo, Fasalejo amekuwa akitumia sanaa yake kusaidia familia yake.

"Ilikuwa ni namna yangu ya kusaidia familia yangu japo mama yangu alinizuia akisema hilo lilikuwa jukumu la wazazi, na sio la Watoto," anasema.

Hata akiwa msanii mchanga, bado alikuwa na hamu kubwa ya kurudisha kwa jamii yake, na kwa mara nyingine akageukia sanaa ili kutoa shukrani zake.

Fasalejo hufurahia kuirudishia jamii kupitia kazi yake./Picha:Fasalejo

"Nilianza kwa kuchora michoro bila malipo kwa watu wa jamii yangu. Nilifanya yote kwenye karatasi ya kawaida na nilipowaonyesha, sura ya shukrani kwenye nyuso zao ilikuwa ya thamani sana,” anakumbuka.

“Niliona ilikuwa ni njia nzuri ya kuwafurahisha.”

Inaridhisha

Moja ya safu yake inayoitwa 'Zaidi ya Hii' ni njia nyingine ya uzuri wa jamii.

“Kuna michoro sita kwenye niliyoitoa kwa jamii yangu,” anaelezea.

“Ni ukumbusho kuwa umoja wetu ndio nguvu yetu.”

Baadhi ya michoro ya msanii huyo./Picha: Fasalejo

Kama ilivyo kwasanii wengine wengi, ubunifu wa Fasalejo huanza na wazo.

Katika mfululizo wake unaoitwa 'Dada ni Baraka' ni ushuhuda wa jinsi msukumo kuongezeka ghafla wakati wa mchakato wa uchoraji.

Simulizi hiyo ilianza kwa uchoraji wa kujitegemea kabla ya kuwa seti ya picha 3," anasema.

Simulizi hiyo ilianza kwa uchoraji wa kujitegemea kabla ya kuwa seti ya picha 3./Picha: Faselejo

Utamaduni na Urithi

Kazi nyingi za Fasalejo huakisi utamaduni na urithi wa Kiyoruba.

“Huashiria changamoto wanazokutana nazo watu na namna ya kukabiliana nazo.”

Kazi nyingi za Fasalejo huakisi utamaduni na urithi wa Kiyoruba/Pıcha: Fasalejo

Mabadiliko ya misimu

Kulingana na Fasalejo, ujuzi wake unatokana na miaka mingi ya mazoezi na masomo pamoja na talanta yake ya asili.

Mafunzo yake katika sanaa nzuri na matumizi pia yalichangia mageuzi yake ya kisanii.

"Kusoma sanaa kulichagiza sana inagwa nilikuwa tayari najua jinsi ya kupaka rangi,” anasema Fasalejo ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Obafemi Awolowo.

Fasalejo amepata nyakati nyingine nyingi za kufurahisha kufuatia kuhitimu kwake ikiwa ni pamoja na mfululizo wake wa 'Muda na Msimu' ambao husherehekea wingi.

"Mfululizo huu maalum una michoro tatu ambazo zote zina asili ya kijani kuashiria hatua tofauti za mageuzi kutoka utoto hadi utu uzima, na hadi wakati hawa watu wazima wana watoto wao au kuwatunza wazazi wao wazee," asema. "Haya yote ni uzoefu wenye matunda sana."

Mafunzo yake katika sanaa nzuri na matumizi pia yalichangia mageuzi yake ya kisanii./Picha: Fasalejo

'Kitu kizuri'

Kazi za Faselejo zimewekwa kwenye maonesho ya picha katika nchi mbalimbali, ikiwemo Kenya na Nigeria.

"Chukua kila fursa kupanua uwezo wako, hata kama ni kufanya kazi nje ya sanaa ambayo huna hamu nayo," anashauri wasanii wanaochipuka.

"Wewe fanya tu na upate uzoefu kwa sababu inaweza kukupa kitu kizuri."

TRT Afrika