Kukatika kwa umeme nchini Ethiopia kuliathiri nyumba, biashara na miundombinu muhimu. / Picha: Reuters

Hitilafu ya umeme nchini Ethiopia, ambayo ilianza mwendo wa saa kumi na mbili jioni saa za huko Jumamosi, ilirejeshwa kikamilifu saa nne usiku Mamlaka ya Nishati ya Umeme ya Ethiopia ilitangaza.

Mamlaka hiyo ilisema kuwa umeme ulirejeshwa taratibu kufuatia takriban saa sita za usumbufu uliosababishwa na "kuyumba kwa mfumo."

Kukatika kwa umeme kuliathiri nyumba, biashara, na miundombinu muhimu, na kusababisha hatua za haraka kutoka kwa mamlaka kutambua na kutatua suala hilo.

Maafisa waliwahakikishia umma kwamba hali sasa imedhibitiwa.

Tukio hili linafuatia tukio kama hilo la Machi 2024, wakati kukatika kwa umeme kwa saa tano kuliingiza sehemu kubwa ya nchi gizani.

Sababu ya kukatika huko haikufichuliwa, na hivyo kuibua wasiwasi unaoendelea kuhusu kutegemewa kwa gridi ya umeme ya Ethiopia.

Mamlaka ya Nishati ya Umeme ya Ethiopia iliwataka wakaazi kuripoti hitilafu zozote za ndani na kuwahakikishia kuwa juhudi za ufuatiliaji zitaendelea kuzuia kukatizwa kwa siku zijazo.

TRT Afrika