Na Pauline Odhiambo
Msanii wa Nigeria Elisha Nyong alikuwa katika shule ya msingi alipoona kwa mara ya kwanza mchoro wa rangi ya mafuta. Akiwa nje ya matembezi siku moja, alikutana na mmoja wa walimu wake akipaka rangi nje na mara moja alifadhaika.
"Ilikuwa picha ya mwanamume aliyeochorwa kwenye picha, na kufanana na mwenye kuchorwa kwa njia isiyokuwa ya kawaida," Elisha anasimulia TRT Afrika.
Kufikia wakati huo, Elisha alikuwa amechukia masomo yake katika sanaa, lakini kumtazama mwalimu wake akichora picha tofauti za rangi ya mafuta mnamo 2007 kulimvutia na mwishowe kukaboresha azimio lake la kuwa msanii.
Lakini Elisha anasema kazi yake katika sanaa ilikuwa ‘wastani’ katika miaka iliyotangulia.
“Baadhi ya wanafunzi wenzangu wangeweza kuchora vizuri zaidi kuliko mimi, na hilo lilinifanya niwe mwanafunzi wa wastani, jambo ambalo, kufikia sasa, halinifurahishi kwa sababu mimi huchukia kuwa wastani katika jambo lolote,” asema msanii wa uhalisia wa kisasa.
''Contemporary ralism",- sanaa ya uhalisia wa kisasa ni mtindo wa kimataifa wa uchoraji ambao ulianza kuwepo katika miaka ya 1960 na mwanzoni mwa miaka ya 70. Kulingana na jukwaa la Art Focus, uhalisia wa kisasa unajumuisha kazi za sanaa za kitamathali zilizoundwa kwa mtindo wa asili uliyokamilika.
Sanaa ya ushindi
Jaribio la kwanza la Elisha la uchoraji wa rangi ya mafuta akiwa na umri wa miaka 14 mnamo 2010 lilimpa nafasi ya juu katika shindano la kitaifa la sanaa.
"Shindano lilipewa jina la 'Art of Guns,' na nilichora kwa jina ‘Niger Delta Crises’ (Migogoro ya Delta ya Niger) ili kuakisi mada, na nilitaka kujadili kuenea kwa uhalifu na shughuli haramu katika eneo hilo," anakumbuka.
Michoro yake mengi yameonyeshwa nchini Nigeria na nchi nyingine nyingi duniani kote ikiwa ni pamoja na Uingereza, Italia, Marekani na Ukraine.
Safari ya Elisha katika sanaa ilimpeleka katika Chuo Kikuu cha Uyo katika jimbo la Akwa Ibom nchini Nigeria, ambako alisomea sanaa ya kiufundi.
Ilikuwa katika chuo kikuu ambapo alikutana na mmoja wa washauri wake Akan David, mtaalamu 'msurrealist' mashuhuri ambaye alibadilisha mtazamo wa Elisha juu ya sanaa.
Mbinu ya kipekee ya Akan ya kujumuisha uhalisia kama mchoro wa kitamathali, na vile vile ishara na mguso wa Pan-Africanism na fumbo, ilikuwa ikimuangazia msanii chipukizi.
"Alinisaidia kuelewa mwingiliano kati ya falsafa na sanaa, na jinsi akili inaweza kuwa kizuizi pekee katika kufikia ubunifu wa hali ya juu," anasema Elisha wa mshauri wake.
Mchoraji mwenye kipawa cha asili
Mtindo wa Elisha ulisifiwa na mfanyakazi mwingine mkuu katika chuo kikuu chake.
Mchoraji huyo mwenye kipawa cha asili, amefanya kazi na vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na rangi ya maji na mkaa lakini kazi yake ya msingi ni rangi ya mafuta.
"Nilikuwa nikiogopa sana picha," asema. "Lakini kwa kutiwa moyo na wenzangu, niliendelea kufanya mazoezi na hatimaye nikakubali mwelekeo wangu wa asili wa kuchora picha."
Miongoni mwa kazi zingine, ni 'Only a memory' imepangwa kuonyeshwa huko Harlem, New York City katika mwezi wa Septemba 2024 kama sehemu ya maonyesho ya 'Black Heroine II'.
Mwanaharakati wa sanaa
"Only a Memory" imechochewa na hali ya sasa ya Gaza, ambapo Israel inaendelea kufanya mashambulizi ya kikatili dhidi ya Wapalestina. Onyesho hilo awali lilipewa jina la ‘Let the Children Play’ kwa heshima ya kumbukumbu kuu ambazo watoto wa Gaza walikuwa nazo kabla ya vita,” Elisha aeleza.
Tangu Oktoba 2023, vita vya Israeli dhidi ya Gaza vimeua zaidi ya Wapalestina 40,000 - wengi wao wakiwa wanawake na watoto - na kujeruhi wengine zaidi ya 93,000 - makadirio ya chini, huku wengine 10,000 wakiaminika kuzikwa chini ya vifusi vya nyumba zilizolipuliwa.
"Msichana katika moja ya picha amevaa joho laini la hariri ambalo linaashiria asili ya kitamaduni ya watu wa Gaza," Elisha anaiambia TRT Afrika.
"Licha ya ukweli kwamba nilimwonyesha katika ngozi ya melanini, ujumbe wa msingi hapa ni kumbukumbu ya maisha mazuri."
Sehemu ya mapato kutoka kwa michoro hiyo yatakwenda kwa watoto wa Palestina.
Picha zenya maana ya ndani
Elisha pia anatumia jukwaa lake la kisanii kushughulikia afya ya akili.
"Picha zangu zimeundwa ili kujadili mada zenye utata kama vile dini, kifo na vipengele vingine muhimu vya hali ya binadamu, ndiyo maana niliweka msingi wa kazi yangu ya 'Black Heroine' kwenye afya ya akili" asema.
"Wasanii wengine hutengeneza picha za kuchora na kisha huitupia tu mada au kupika falsafa kwa hiyo, ambayo ninahisi kuwa ya ulaghai kwangu," anaongeza Elisha.
"Kama mbunifu, sikubaliani na hilo kwa sababu sitaki kuwa msanii mwingine wa kibiashara wa Kiafrika anayeiga mtindo kwa sababu ni maarufu."
Lakini ufasaha katika kueleza mafumbo haukuwa ufahamu wa mara moja kwa Elisha.
"Watu wanasema kwamba kila kitu huja kawaida mara tu unapohitimu chuo kikuu, lakini hiyo haikufanyika kwangu," msanii huyo ambaye alipata digrii yake ya bachelor mnamo 2017.
"Nilikuwa nikichora mandhari na chochote kingine nilichohisi kama kupaka rangi kwa sababu sikuwa na mtindo wangu binfasi wa uchoraji."
Sauti za ndoto
Wakati wa kufahamu mtindo wake wa kisanii hatimaye ulimjia mnamo 2022.
"Nilirudi kwenye karatasi niliyochapisha katika chuo kikuu kama mwanafunzi wa shahada ya kwanza. Karatasi hiyo imepewa jina la 'Surrealism and the Psyche: Unlocking the Creative-self; kushughulikia matatizo ya kisaikolojia yanayowakabili wasanii na wabunifu kwa ujumla,” anaiambia TRT Afrika.
"Kwa kuwaza ya nyuma, nilitafakari kwa kina kuhusu kila kitu nilichokuwa nacho kwenye karatasi hiyo, na kisha siku moja nikapata ujasiri wa kuunda mifululizo ya michoro nilioupa jina la 'Echoes of a Dream,'," asema msanii huyo.
“Kipande cha kwanza kwenye mkusanyo huo kilinunuliwa hata kabla sijamaliza. Hiyo ilikuwa miaka miwili iliyopita, na tangu wakati huo, kila kitu kimetokea kwa kawaida kulingana na utambulisho wangu wa kisanii."
Sanaa ya Elisha sasa inauzwa kwa maelfu ya dola katika soko la kimataifa.
Kwa sasa anawakilishwa na Jumba la sanaa la Constance and Sons nchini Nigeria na Jumba la Sanaa la Juu huko Seattle, Marekani, na Omíníra Art &Tea huko Harlem, NYC.
Ushauri wake kwa wasanii wanaotarajiwa: "Ufunguo wa kufanikiwa ni uthabiti. Chapa kubwa zaidi ulimwenguni haziuzi bidhaa, zinauza uthabiti, na katika usanii, uthabiti ni muhimu ili kusalia kuwa muhimu."