Chama cha DP ndiyo upinzani rasmi kwa chama tawala Afrika Kusini, African National Congress (ANC), chama kikuu katika siasa za Afrika Kusini, na pia cha pili kwa ukubwa / Picha: Reuters

Chama cha Democratic Alliance (DA) ni chama cha kisiasa nchini Afrika Kusini.

Ndiyo upinzani rasmi kwa African National Congress (ANC), chama kikuu katika siasa za Afrika Kusini, na pia cha pili kwa ukubwa. DA iliundwa mwaka 2000.

Historia ya DA inaanza na Democratic Party (DP). DP ilianzishwa mwaka 1989 wakati Progressive Federal Party, National Democratic Movement, na Independent Party zilipounganishwa.

Hii ilikuwa wakati wa ubaguzi wa rangi, wakati Waafrika Kusini weusi hawakuruhusiwa kupiga kura.

DP iliunga mkono wazo la kuwapa watu weusi wa Afrika Kusini haki ya kupiga kura.

Pia iliunga mkono mabadiliko ya katiba ambayo yangefanikisha lengo hili.

Wanafuasi wa chama cha DA wakiwa katika kampeni za uchaguzi wa 2024 huko Soweto, Afrika Kusini/  Picha: Reuters 

Katika uchaguzi mkuu wa 1994, baada ya ubaguzi wa rangi kumalizika, chama cha DA kilipata viti saba pekee katika Bunge la Kitaifa. Hii iliwaweka nyuma sana ANC.

Lakini mwaka 1999 DP ilishinda viti 38 na kuwa chama cha pili kwa ukubwa katika bunge hilo. Mwaka mmoja baadaye DP ilijiunga na New National Party (NNP) na Muungano wa Shirikisho kuunda Muungano wa Kidemokrasia.

Lengo lilikuwa kuunda mpinzani mwenye nguvu zaidi kwa ANC. Lakini muungano kati ya pande hizo tatu ulikuwa mfupi. Mwaka 2001 NNP iliondoka na kuunda muungano na ANC.

Kiongozi wa DA John Steenhuisen

John Steenhuisen alizaliwa mwaka wa 1976.

Aliteuliwa kuwa Kiongozi wa chama cha DA katika Kongamano la Shirikisho la DA la 2023 tarehe 2 Aprili 2023.

John Steenhuisen aliteuliwa kuwa kiongozi wa chama cha DA Aprili 2023/ Picha: Reuters 

John hapo awali alichukua nafasi ya kiongozi wa muda wa Shirikisho kuanzia Novemba 2019, akiwa amehudumu kama Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuanzia Mei 2014 hadi Oktoba 2019.

John amekuwa mwakilishi wa umma kwa zaidi ya miaka 20. Amekuwa mjumbe wa Bunge tangu Julai 2011.

Chama hiki cha Democratic Alliance (DA), kilikuwa cha pili kwa wingi wa kura katika uchaguzi mkuu Afrika Kusini 2024, kwa asilimia 21.81.

Chama tawala cha Afrika Kusini Africa National Congress, ANC kiliongoza na 40.18% lakini kikakosa kufikia mahitaji ya 51% inayohitajika na katiba ya nchi hiyo ili iunde serikali.

Muungano na Chama cha DA unaangaliwa kama suluhu kwa chama tawala cha ANC kuunda serikali ya pamoja.

TRT Afrika