Waasi hao wamezidi kusonga mbele kupata upinzani wowote kutoka jeshi la serikali la DRC./Picha: Getty

Burundi imeanza tena kutuma vikosi vyake vya kijeshi mashariki mwa DRC, kusaidia jeshi la nchi hiyo dhidi ya waasi wa M23.

Hatua hiyo inakuja wakati waasi wa M23, wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda wakiendelea kutwaa na kudhibiti miji yenye hifadhi kubwa ya madini nchini humo.

Waasi hao wamezidi kusonga mbele kupata upinzani wowote kutoka jeshi la serikali la DRC.

Wakati kikundi cha M23 kikisonga kuelekea mji wa Uvira ulio kaskazinimagharibi mwa Ziwa Tanganyika, wanajeshi wa Burundi walikuwa wakielekea kaskazini mwa Uvira, kujaribu wa kuwadhibiti waasi hao.

"Toka Jumapili, tumeshuhudia majeshi ya Burundi wakielekea Luvungi", baadhi wakitembea kwa miguu kutoka Uvira, na wengine wakivuka mto Ruizi ambao uko katika mpaka wa DRC na Burundi,” alisema mkazi mmoja wa eneo la Sange nchini DRC.

Inadaiwa kuwa, wanamgambo waitwao Wazalendo, wenye kuunga mkono jeshi la DRC wanaungana nao katika eneo la Luvungi, alidai mkazi mwengine kwa sharti la kutotajwa jina.

Hayo yanajiri baada ya wanajeshi wa Afrika Kusini, waliojeruhiwa katika machafuko hayo kurudishwa nyumbani kwa matibabu.

Wanajeshi hao, walikuwa sehemu ya vikosi maalumu kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) waliotumwa nchini DRC toka mwaka 2023, kwa ajili ya shughuli ya ulinzi mwa amani.

TRT Afrika