Salamu za rambirambi zimetolewa kufuatia kifo cha mwandishi wa vitabu na mshairi maarufu nchini Afrika Kusini, Breyten Breytenbach.
Breytenbach alisifika sana kwa uhodari wake wa kucheza na maneno, akiwa ni sauti ya fasihi ya Kiafrikaana, na mwiba mkali dhidi ya sera ka kubaguzi.
"Ni huzuni tunapomkumbuka Breyten Breytenbach kwa ujasiri wake wa kupambana na mateso ya ubaguzi wa rangi,” aliandika Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kwenye ukurasa wake wa X siku ya Jumatatu.
Kinara
Meya wa Cape Town Geordin Hill-Lewis, alimuelezea Breytenbach kama “gwiji wa mashairi.”
“Breytenbach alikuwa kinara kwenye fasihi ya Afrika Kusini tu bali ulimwengu mzima,” aliongeza.
Breytenbach alihamia jijini Paris, akikamatwa mwaka 1975 wakati akiwa nchini Afrika Kusini, akishitakiwa kwa uhaini na kulazimika kutumikia kifungo cha miaka saba jela.
Alihamia Paris baada ya kuachiwa huru, huku akiendeleza harakati zake dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Kazi maarufu
Breytenbach alipokea tuzo nyingi, maarufu zaidi zikiwa Tuzo la Van der Hoogt la Fasihi ya Kiholanzi mnamo 1982, ambayo ilifuatiwa na Tuzo ya Fasihi ya Rapport mnamo 1986.
Pia alipokea Tuzo la Kimataifa la Fasihi la Zbigniew Herbert, Tuzo la Kitabu la Anisfield-Wolf, na Tuzo la Alan Paton la Fasihi, miongoni mwa mengine.