Miaka mitanu iliyopita Botswana ilitangaza kupata almasi ya tatu kwa ukubwa duniani/ Picha: AFP

Botswana inasema moja ya almasi kubwa kuwahi kupatikana imechimbuliwa katika migodi yake.

Kampuni ya uchimbaji madini ya Canada ya Lucara Diamond Corp. ilisema katika taarifa yake Jumatano kwamba ilipata almasi "ya kipekee" kutoka Mgodi wake wa Karowe uliopo magharibi mwa Botswana.

Lucara alisema lilikuwa jiwe la "ubora wa juu" na lilipatikana likiwa katika hali nzuri kwa kutumia teknolojia ya X-Ray.

Uzito huo ungeifanya kuwa almasi kubwa zaidi kupatikana katika zaidi ya miaka 100 na ya pili kwa ukubwa kuwahi kuchimbwa mgodini baada ya Almasi ya Cullinan kugunduliwa nchini Afrika Kusini mwaka wa 1905.

Almasi ya dola milioni 53

Cullinan ilikuwa na karati 3,106 na ilikatwa kuwa vito, ambavyo baadhi ni sehemu ya Vito vya taji ya Mfalme wa Uingereza.

Almasi kubwa nyeusi iligunduliwa nchini Brazili mwishoni mwa miaka ya 1800, lakini ilipatikana juu ya uso na iliaminika kuwa sehemu ya 'meteorite' au miamba ya anga ambayo huanguka duniani.

Botswana ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa almasi na imefukua mawe yote makubwa zaidi duniani katika miaka ya hivi karibuni.

Kabla ya ugunduzi huu, almasi ya Sewelo, ambayo ilipatikana katika mgodi wa Karowe mnamo 2019, ilitambuliwa kama almasi ya pili kwa kuchimbwa kwa ukubwa duniani kwa karati 1,758.

Almasi ya Lesedi La Rona yenye karati 1,111, pia kutoka Mgodi wa Karowe wa Botswana, ilinunuliwa na sonara wa Uingereza kwa dola milioni 53 mwaka 2017.

Almasi mpya iliyogunduliwa Botswana itaonyeshwa wazi katika ofisi ya Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi, serikali ya Botswana ilisema. Masisi atakuwa wa kwanza kuiona.

TRT Afrika