Zaidi ya watu 151,000 wamekimbilia majimbo jirani, ikiwa ni pamoja na Gedaref/ Picha kutoka NRC

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yametoa tahadhari kuhusu kuongezeka kwa njaa nchini Sudan.

Mashirika hayo ni pamoja na Norwegian Refugee Council, Danish Refugee Council na Mercy Corps.

" Sudan inakabiliwa na baa kubwa la njaa huku ukimya mkubwa ukitawala suala hili. Watu wanakufa kwa njaa, kila siku, na bado majadiliano yamesalia kama mijadala tu," yamesema mashirika hayo.

Mashirika haya yamezindua ripoti iitwayo "If Bullets Miss, Hunger Won't".

Vita kati ya jeshi la Sudan na kikundi cha Rapid Support Forces vimekuwa vikiendelea tangu mwezi Aprili 2023.

Zaidi ya watu milioni 25 nchini humo wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula huku familia nyingi zikipitisha siku kwa mlo mmoja na wengine kulazimika kula majani au wadudu.

Baadhi ya watu wa kujitolea wamekuwa wakisaidia kulisha jamii zilzokumbwa na uhaba wa njaa./ Picha NRC

Ripoti hiyo inaongeza kuwa watu wa Sudan wameonesha ujasiri na nguvu kubwa katika kipindi cha miezi 17 iliyopita, ila kwa sasa hawana pa kukimbilia.

Chanzo cha njaa ni wanadamu

Kulingana na ripoti hiyo, ukosefu wa usalama nchini humo umevuruga utaratibu mzima wa upatikanaji wa chakula, huku watu wengi wakilazimika kuyahama makazi yao.

Mashirika yamezuiliwa kutoa misaada ya kibinadamu, na kwa makusudi kuzuia upatikanaji wa misaada kwa mamilioni ya watu wenye uhitaji mkubwa

Kwa mujibu wa mashirika hayo, njaa sio sababu pekee ya kutokea kwa migogoro hiyo, bali imechangiwa pia na kutozingatia sheria za kimataifa.

Mashirika hayo, pia yameongeza kuwa viongozi wa nchi hiyo wameshindwa kulinda raia, miundombinu muhimu, pamoja na ikiwa ni pamoja na chakula, na hivyo misaada kuwafikia kwa wakati.

" Matokeo yake ni njaa kuwa silaha ya vita," imesema ripoti hiyo.

UN yataka vikwazo vya silaha nchini Sudan

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mapigano kati ya Jeshi la Sudan na kikundi cha Rapid Support Forces vimesababisha dhuluma kubwa ambayo inaweza kutafsiriwa kama uhalifu wa kivita au uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Ripoti hiyo yenye kurasa 19 za Ujumbe wa Kutafuta Ukweli wa Umoja wa Mataifa, ilitokana na mahojiano 182 yaliyofanywa pamoja na manusura wa machafuko hayo, familia zao na mashahidi, pia ilidai kuwa Jeshi la Sudan na kikosi cha RSF vilihusika na mashambulizi dhidi ya raia, mateso na ukamataji wa watu kiholela.

"Uzito wa matokeo haya unasisitiza hatua za haraka na za haraka za kulinda raia," Mwenyekiti wa ujumbe huo Mohamed Chande Othman, akitoa wito kwa kikosi huru kutumwa Sudan.

Ripoti hii ni ya kwanza ya ujumbe huo wa wajumbe watatu tangu kuundwa kwake Oktoba 2023 na Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT Afrika