Benki Kuu ya Tanzania katika taarifa yake iliyotolewa Mei 13, imewatahadharisha wale wanaojihusisha na biashara ya kukopesha ka njia ya kidigitali kuhakikisha wanapata leseni ya biashara hiyo kutoka Benki Kuu.
"Kwa mujibu wa kifungu cha 16 (1) cha sheria, ni kinyume cha sheria kujihusisha na biashara ya kukopesha bila kuwa na leseni," imesema taarifa ya Benki Kuu, na kuongeza kusema kuwa katazo hilo pia linajumuisha utoaji wa mikopo kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa njia ya kidijitali bila kuwa na leseni.
Hatua hii inakuja siku chache kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa bunge na baadhi ya wabunge, wakihoji uhalali wa baadhi ya watu na taasisi binafasi ambazo zinajikita katika utoaji wa mikopo kidijitali kila kuzingatia miongozi iliyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania.
Aidha, wananchi pia wametakiwa kusoma kwa makini na kuelewa vipengele vyote vya makubaliano wanayoingia na wakopeshaji.