Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres and Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat wameongoza mashirika yao katika mkutano wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, huko New York nchini Marekani.
Viongozi hao wawili, waliongelea suala la vikosi vya kulinda amani ambavyo vimekuwa chanzo cha utata katika sehemu tofauti barani Afrika.
Kumekuwa na wimbi wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa barani Afrika, vikilaumiwa kutokuwa na umuhimu wowote.
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanahudumu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mali, Sahara Magharibi, Sudan Kusini.
Nchini Sudan, kuna ujumbe mmoja huko Darfur (pamoja na Umoja wa Afrika) na mmoja katika eneo linalozozaniwa la Abyei.
"Jinsi yalivyo sasa, mamlaka ya ujumbe huu hauendani na asili ya changamoto ambazo mara nyingi tunaziona barani Afrika," Moussa Mahamat Faki, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika amesema.
Watu wamekosa imani kwa vikosi vya UN
Nchini Mali, vikosi vya Umoja wa Mataifa, MINUSMA, vinajioondoa baada ya serikali ya Mali kuitaka iondoke Juni tarehe 30, mamlaka yake ikimalizika.
MINUSMA ilianzishwa Aprili 25, 2013, ili kukabiliana na mzozo wa usalama uliozuka nchini Mali.
Ujumbe huu ulihusisha zaidi ya askari 15,000 na maafisa wa polisi kutoka nchi 61, kuanzia Armenia hadi Zambia. Kikosi cha kulinda amani kimsingi kilikuwa kaskazini na katikati mwa Mali.
"Nchini Mali, tumekuwa tukisema kwamba kulikuwa na uwezekano wa tishio la kaskazini mwa Mali kuenea katika nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Burkina Faso. Kwa kuangalia tu mfano huo, nadhani ni kawaida kabisa kwa kukagua hali hiyo," ameongezea.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia imeamuru kikosi cha walinda amani cha UN kuondoka nchini mwake.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuimarisha Udhibiti wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) kwa miaka 25.
"Ni wakati wa nchi yetu kuchukua udhibiti kamili wa hatima yake na kuwa mhusika mkuu katika utulivu wake," rais wa DRC, Felix Tshisekedi aliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba 2023.
Ujumbe huo ulitia saini makubaliano Novemba kuondolewa kwa wanajeshi wake nchini humo.
Mkataba huo umetiwa saini na Bintou Keita, Mkuu wa MONUSCO na Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Christophe Lutundula, wakisema vikozi hivyo vitaondoka katika awamu tatu.
"Mtazamo wetu katika Umoja wa Afrika, na hili ni jambo ambalo linakubaliwa na katibu wa Umoja wa Mataifa, ni kwamba, asili ya vitisho hivi ambavyo tunaviona barani Afrika vinahitaji kupata jibu linalofaa. Tumependekeza kuunda vikosi vyetu, lakini vikosi hivi vinahitaji kufadhiliwa na bajeti ya Umoja wa Mataifa."
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres anasema ujumbe wa kulinda amani una mantiki ya kuleta utulivu baada ya mchakato wa amani kufanyika.
"Tunapokuwa na hali kama ile tuliyo nayo Mali au ile tuliyo nayo katika maeneo mengine yaliyoathiriwa na ugaidi, tunachohitaji ni kutekeleza amani na operesheni za kukabiliana na ugaidi," Gutters amesema.
"Tunahitaji operesheni za kuleta amani na kupambana na ugaidi barani Afrika, ikiongozwa na Umoja wa Afrika," Gutteres aliambia waandishi wa habari.
Mtazamo wetu katika Umoja wa Afrika, na hili ni jambo ambalo linashirikiwa na SG, ni kwamba asili ya vitisho hivi ambavyo tunaviona barani Afrika vinahitaji kuona jibu linalofaa. Tumependekeza kufanya vikosi vyetu vipatikane, lakini vikosi hivi vinahitaji kufadhiliwa na bajeti ya Umoja wa Mataifa. Hili ni tishio kwa amani na usalama, na kwa hivyo, ni jukumu la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Nadhani kwamba, bila shaka, kila hali inahitaji majibu kulengwa. Pale ambapo mabadiliko yanahitajika, basi mabadiliko haya yanatakiwa kutekelezwa. Nadhani ndivyo tunavyotarajia.
Sasa mjadala, leo ni kuhakikisha kwamba Baraza la Usalama linakubali ufadhili unaohitajika ili shughuli hizi ziwe hivyo.
na kwa mamlaka kamili ya Baraza la Usalama chini ya Sura ya VII. na kutathmini michango ya kufadhili misheni hizo. Ndio njia pekee ya kuwa na ufanisi katika kupambana na aina ya vurugu na ugaidi ambao sasa unaenea katika nchi nyingi za Afrika.