Grace Naledi Mandisa Pandor, Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano, Afrika Kusini akihutubia mkutano wa Antalya Diplomacy Forum / Picha : Antalya Diplomacy Forum 

Na Coletta Wanjohi

TRT Afrika, Antalya, Uturuki

Mkutano wa kimatifa wa majadiliano ya kidiplomasia yaani Antalya Diplomacy Forum umekamilika.

Mkutano huo uliokuwa ukifanyika mjini Antalya nchini Uturuki kuanzia tarehe 1 hadi 3 Machi mwaka huu, umesisistiza umuhimu wa kutumia mbinu zisizo za kivita kwa ajili ya kutatau changamoto duniani.

Wahusika kutoka Afrika na sehemu nyingine duniani walihudhuria mkutano huu wa kila mwaka ulioandaliwa na serillai ya Uturuki.

Afrika Kusini imeendelea kupaza sauti kwa ajili ya Palestina, ikisema kuwa ni lazima dunia iunge mkono swala la Wapelestina kupata haki yao dhidi ya mashambulizi kutoka Israeli.

“Hatukuabaliani kwamba Israel inajikinga kwa mashambulizi kutoka kwa Wapalestina, hapana, Israel inafanya mauaji,” Grace Naledi Mandisa Pandor, Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano, Afrika Kusini ameiambia TRT Afrika.

Afrika Kusini iliishitaki Israel katika mahakama ya Kimataifa ya haki, kwa mauaji ya kimbari ya Wapalestina.

Lakini hata baada ya mahakama kuamuru Israel kusitisha mashambulizi bado Israel inaendelea.

“Haya yote sio halali, wananyakua ardhi ya Wapalestina ambao hawafania maovu yoyote dhidi ya watu wa Israel, ”Waziri Naledi ameambia TRT Afrika.

"Tuna tofauti katika eneo la Kusini mwa ulimwengu, lakini jambo moja linalotuunganisha wote ni historia ya ukandamizaji na ukoloni. Hiki ndicho kinachotuunganisha katika mapambano ya Palestina.”

Afrika Kusini imetoa wito katika mkutano wa Antalya Diplomacy Forum kwa jamii ya kimataifa kuhalalisha serikali ya Palestina .

“Jamii ya Kimataifa inafaa kufanya mengi zaidi kwa ajili ya kusitisha vita na hapo baadaye suluhisho itafutwe kwa uundaji wa nchi mbili,” Naledi amesisistiza.

TRT Afrika