Zoezi la upiga kura linaendelea nchini Afrika Kusini./Picha:Reuters

Afrika Kusini imeanza zoezi la uchaguzi siku ya Jumatano, mchakato unaolezwa kuwa muhimu zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Macho na masikio ya wengi katika uchaguzi huo yatakuwa kwenye chama tawala cha ANC, kilichosaidia kuondolewa kwa utawala wa kibaguzi mwaka 1994. Hata hivyo, takribani watu milioni 62 nchini humo wanaishi kwenye dimbwi la umasikini.

Nchi hiyo yenye uchumi mkubwa barani Afrika inakumbana na changamoto za kijamii na kiuchumi ikiwemo ukosefu wa ajira kwa kiwango cha asilimia 32.

Kukosekana kwa usawa, umaskini na ukosefu wa ajira kwa kiasi kikubwa umeathiri watu wengi na unatishia kukiondoa chama cha ANC kilichoondoa ubaguzi wa rangi chini ya kauli mbiu ya maisha bora kwa wote.

Baada ya uchaguzi wa mara sita mfululizo, michakato kadhaa imeonesha ANC kuungwa kwa chini ya asilimia 50 kuelekea uchaguzi huo. Chama hicho kinatarajiwa kupoteza nafasi nyingi za ubunge.

Chama hicho kinazidi kupoteza ushawishi. ANC ilishinda asilimia 57.5 ya kura zote kwenye uchaguzi wa 2019, matokeo mabaya zaidi ya chama hicho.

Hata hivyo, Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa, ambaye pia ni kiongozi wa ANC aliahidi ''kufanya vyema zaidi.” Chama hicho kimewaomba wafuasi wake kuwa na subira zaidi.

Mabadiliko yoyote katika kushikilia madaraka kwa ANC yanaweza kuwa makubwa kwa Afrika Kusini. Iwapo itapoteza wingi wake, ANC itakabiliwa na uwezekano wa kuunda muungano na wengine ili kusalia serikalini na kumbakisha Ramaphosa kama rais.

Uchaguzi huo unafanyika kwa siku moja ndani ya majimbo tisam huku watu milioni 28 wakiwa wamesajiliwa kupiga kura katika vituo 23,000. Matokeo ya jumla ya mchakato huo yanatarajiwa kutolewa siku ya Jumapili. Ramaphosa alitarajiwa kupiga kura yake mapema leo katika mji mdogo wa Soweto ndani ya Johannesburg.

AP