Jaciob Zuma alihudumu kama Rais wa Afrika Kusini, kuanzia 2009 hadi 2018./Picha: AP

Katika taarifa yake ya Jumapili, Makahama ya Katiba ya nchi hiyo imesema kuwa itatoa hukumu ya iwapo Zuma anastahili kugombea kufuatia kesi yake ya Juni 2021.

Ili mgombea afuzu kwa kiti cha urais nchini Afrika Kusini, ni lazima awe amehitimu kuhudumu kama mbunge.

Zuma alipewa hukumu ya miezi 15 jela kwa kukaidi kutoa ushahidi kwa tume inayochunguza tuhumu za ufisadi dhidi yake, wakati akiwa Rais wa Afrika Kusini, kati ya 2009 na 2018.

'Upendeleo'

Katika uamuzi wake wa Jumatatu, mahakama ya kikatiba pia itajibu swali: "Iwapo tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ilivuka mamlaka yake katika kuamua kama Zuma anastahili kugombea katika Bunge la Taifa.

Mwishoni mwa mwezi Machi, Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini (IEC) ilimzuia Zuma kugombea katika uchaguzi wa rais wa Mei 29 kutokana na kudharau hukumu yake ya mahakama, ambayo ilimweka Zuma jela kwa zaidi ya miezi 12, kifungo gerezani ambacho kina muondolea sifa ya kugombea, kulingana na katiba ya Afrika Kusini.

Hata hivyo, uamuzi huo ulibatilishwa na mahakama ya uchaguzi ya nchi hiyo juu ya ombi la Zuma, na kusababisha IEC kuwasilisha rufaa katika mahakama ya kikatiba.

Miongoni mwa mambo mengine, siku ya Jumatatu, mahakama hiyo itatoa uamuzi kuhusu iwapo tume ya uchaguzi ilionesha "uwepo wa upendeleo".

Mchuano wake na Rais aliye madarakani

Zuma, ambaye alikuwa mwanachama wa chama tawala cha ANC kwa takriban miaka 65 kabla ya kukiacha Desemba 2023, anakusudia kugombea urais kupitia chama chake kipya, uMkhonto weSizwe (MK).

Iwapo ataruhusiwa kugombea, Zuma atachuana na Cyril Ramaphosa kutoka ANC, ambaye anakabiliwa na kazi kubwa ya kuongeza idadi ya ANC.

TRT Afrika