Raia wa Afrika Kusini husherehekea 'Siku ya Uhuru' kila Aprili 27, wanapokumbuka uchaguzi mkuu wa kwanza wa kidemokrasia nchini mwao mwaka 1994 ambao ulitangaza kumalizika rasmi kwa ubaguzi wa rangi na ukandamizaji chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi wa Wazungu wachache.
Jumamosi ni kumbukumbu ya miaka 30 ya kura hiyo muhimu, wakati mamilioni ya Waafrika Kusini Weusi, vijana kwa wazee, waliamua mustakabali wao wenyewe kwa mara ya kwanza, haki ya kimsingi ambayo walikuwa wamenyimwa na serikali ya Wazungu wachache kwa miongo kadhaa.
Uchaguzi wa kwanza wa rangi zote ulishuhudia chama kilichopigwa marufuku hapo awali cha African National Congress kikishinda kwa wingi kumpa mamlaka rais wa kwanza Mweusi nchini humo.
Kubadilisha Afrika Kusini
Takriban Waafrika Kusini milioni 20 wa rangi zote walipiga kura, ikilinganishwa na Wazungu milioni 3 pekee katika uchaguzi mkuu uliopita chini ya ubaguzi wa rangi mwaka 1989.
Ushindi wa uchaguzi wa ANC ulihakikisha kwamba ubaguzi wa rangi hatimaye ulivunjwa na Katiba mpya ikaundwa na kuwa sheria ya juu kabisa ya Afrika Kusini, inayohakikisha usawa kwa kila mtu.
Rais wa sasa wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ataongoza maadhimisho ya Siku ya Uhuru ya kuadhimisha miaka 30 Jumamosi katika Majengo ya Muungano huko Pretoria, makao makuu ya serikali.
''Ni muhimu kwamba tuchukue muda kutafakari kile ambacho serikali inayoongozwa na ANC imefanya katika juhudi zake za kubadilisha nchi hii kuwa bora,'' Ramaphosa alisema Ijumaa kabla ya maadhimisho hayo.
Somo kutokana na siku hii
Chama cha ANC kimekuwa serikalini tangu 1994 na wakati bado kinatambulika kwa jukumu lake kuu katika kuwakomboa Waafrika Kusini, hakikumbukwi tena kwa njia sawa na ilivyokuwa katika matokeo yaliyojaa matumaini ya uchaguzi huo wa kwanza.
Afrika Kusini mwaka 2024 ina matatizo makubwa ya kijamii na kiuchumi. Kiwango rasmi cha ukosefu wa ajira ni 32%.
Lakini Ramaphosa alisema Waafrika Kusini lazima watafakari ili waweze ''kupata mafunzo na kupanga kwa ajili ya siku zijazo.''
Muungano unaowezekana
Maadhimisho ya miaka 30 ya 1994 yanaangukia na uchaguzi mwingine unaoonekana kuw amuhimu sana.
Afrika Kusini itapiga kura yake ya saba tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi Mei 29, huku kura zote za maoni na wachambuzi wakitabiri kuwa ANC itapoteza wingi wake wa wabunge katika alama mpya.
ANC bado kinatarajiwa kuwa chama kikubwa zaidi na huenda kitalazimika kuingia katika miungano na vyama vidogo ili kubaki sehemu ya serikali.