Mwishoni mwa mwezi Julai ulikuwepo kwenye ziara ya Rais Macron nchin Cameroon, Benin na Guinea-Bissau. Ni kipi hasa uling’amua na kuwasilisha katika mkutano wa kilele kuhusu Afrika na Ufaransa? Yapo masuala kadhaa niliyoshughulikia; moja ni kuhusu mchakato wa mpito nchini Cameroon. Rais Paul Biya ameliongoza taifa hilo kwa miaka 40 na hilo halimaanishi kuwa ndiye anayeweza kuongoza tu. Taifa hilo linakumbwa na changamoto nyingi na hivyo basi mchakato wa mpito sharti ufanyike kwa njia ya amani. Ufaransa kama mshirika wa karibu wa Cameroon inapaswa kuhusika basi kwenye mazungumzo kupisha uongozi mpya. Maswali yanayohusu kumbukumbu za vita vya kujinyakulia uhuru vilevile yalipaswa kuwasilishwa. Taifa la Benin nalo kwa sasa linazingatia sana utalii na liko tayari kufungua milango yake zaidi kwa watalii. Urejeshaji wa sanaa na serikali ya Ufaransa kwenye makumbusho ya Cotonou ni jambo lingine pia nilitaka kushuhudia. Kwa kuzingatia ukosoaji mkubwa unaokumbana nao katika kazi zako kama msomi wa masuala ya uongozi hasa baada ya ukoloni, unawezaje kutekeleza ipasavyo wajibu wako ikizingatiwa kuwa tupo katika nyakati ambazo chaguo la upande mmoja lazima lifanyike? Ni muhimu sana kujiepusha na tabia hii ya kuegemea upande mmoja. Nachomweleza Rais Emmanuel Macron ni kile ambacho nimekiandika kweye vitabu vyangu. Siongezi na wala sipunguzi. Sibadiliki eti kisa nimepewa wadhifa. Hapana. Mipaka ama vigezo vyako ni gani mtu anapokubali kazi kama hii yako? Mipaka ni kujifahamu wewe mwenyewe. Haihusiana vyovyote na umma. Ni nafasi adhimu sana. Binafsi nimejiweka wazi – katika vitabu vyangu vilivyotafsiriwa kwa lugha tofauti. Ukweli na udhabiti huo ndiyo naodhihirisha pia hata napokutana na Rais wa nchi au kwenye majukwaa nayoalikwa kutoa mchango wangu. Siri iko katika kujiamini, kufikiria na kuwa mkweli kwenye kufanya maamuzi siku zote pasi ya kushawishika. Unapozungumzia nguvu hio ya kufikiria na kujiamini mwenyewe, mawazo yako mara nyingine yanakwenda kinyume na mawazo ya walio wengi; na ukweli ni kwamba dhana ya “sisi” ina nguvu sana nyakati hizi. Bila shaka tupo katika nyakati ambazo dhana hio ya “sisi” ina nguvu kubwa lakini ili kujenga jamii dhabiti basi ni lazima watu wakumbatie utayari wa kufikiria kwa makini. Kwa bahati mbaya mitandao ya kijamii imedidimiza hilo kwa kiwango kikubwa hapa Afrika. Muhimu kwangu ni kuona uhusiano wa Afrika na Ufaransa ukiimarika pasi ya kutawaliwa na hisia za kitoto zisizokuwa na tija.
Mlikuwepo Cameroon mwezi Julai kisha Algeria mwezi Agosti – nchi mbili zilizo na historia chungu ya kupigania uhuru wao dhidi ya Wafaransa. Unachukuliaje ziara hizi za Macron katika mataifa hayo?
Tunaishi katika dunia ambayo watu hawataki kufanya mazungumzo. Watu hawataki kuzungumza na maadui. Mazungumzo yamegeuzwa kuwa usaliti. Je, hii ndiyo aina ya dunia tunayoitaka? Binafsi sitaki.
Hata viongozi wa vuguvugu la kupigania Uhuru kama Patrice Lumumba na Ruben Um Nyobe waliomba mazungumzo. Kiongozi kama Nelson Mandela angekataa kuzungumza na maadui zake sijui Afrika Kusini ingelikuwa wapi sasa hivi. Ni sharti tuheshimu nguvu ya mazungumzo. Kwa mfano Rais Macron anapozuru Algeria bila shaka anahitaji gesi nayo Algeria inahitaji kuuza gesi yake. Chaguo lililobaki ni kumjenga mwenzako.
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umepelekea baadhi ya wachanganuzi kama Bertrand Badie kusema kuwa mataifa yenye nguvu yako sawa sasa hivi “kihatari,” kumaanisha kuwa huenda hilo likaiweka Afrika kwenye “sehemu ya nguvu” kutokana na changamoto ya mafuta na nishati. Je, unaweza ukasema kuwa mzozo ulioko Ukraine unachochea historia kama ilivyokuwa hali kipindi cha COVID?
Bertrand yupo sahihi. Sote sasa hivi tumo hatarini lakini kiwango cha hatari hiyo hakifanani kama tu tulivyoshuhudia kwenye suala la upatikanaji wa chanjo za COVID. Hatuna budi kushirikiana iwapo tunataka mafanikio.
Ushirikiano kati ya mataifa sharti urejee kwenye ajenda; tunataka kuona China ikizungumza na Marekani, Urusi izungumze na Marekani ama NATO nayo Ulaya izungumze na Afrika…..
Kwa hivyo tuseme inampasa mtu kuzungumza na kila mtu?
Kuna mbadala wa hilo kweli? Ama ni tupigane mpaka vita vya nyukilia? Hilo ndio chaguo tu tulilobaki nalo kweli?
Mwezi Julai Turkiye ilifanikiwa kushawishi Ukraine na Urusi kutia saini makubaliano ya kurejelea uuzaji wa nafaka. Je, Ulaya inaweza kushinda uadui ulioko dhidi ya Türkiye kwa faida yake mwenyewe? Makubaliano hayo yanazuia kuwepo kwa njaa barani Afrika na dunia kwa ujumla.
Kwa kweli maslahi haya sio kwamba hayawezi kuambatana. Yanaweza. Hilo ndilo jukumu la diplomasia na hivyo basi mazungumzo ni muhimu.
Türkiye ina maslahi barani Afrika lakini pia Afrika ina maslahi yake na inataka kufanya biashara na Turkiye. Tunahitaji dunia ambayo kila mmoja anapata chake na wala sio kumtumia mwenzake kwa maslahi yake mwenyewe. Huo ndiyo mtihani mkubwa kwa ustaarabu katika karne hii ya 21.
Suala kuhusu semi na kauli za kuikosoa Ufaransa linahitaji uchanganuzi wa kina. Zipo sababu za kihistoria na kiuchumi. Hali kadhalika asasi za kiraia barani Afrika zinapaswa kuchochea fikra chanya miongoni mwa watu ili wadadisi uongozi na siasa kwa kuzingatia maadili.
Kuhusu mzozo wa Urusi na Ukraine, Rais Macron alizidi kuwasiliana na Vladimir Putin lakini ni wazi kuwa mazungumzo hayo hayakuwa na ufanisi mkubwa; lakini cha muhimu zaidi ni kwamba alifanya juhudi kuwasiliana na mwenzake.
Mwaka 2020 nchini Ujerumani, ilidaiwa kuwa ulitoa kauli za kibaguzi dhidi ya Wayahudi kwa kulinganisha mfumo wa ubaguzi wa rangi wa Apartheid Afrika Kusini na masaibu ya Wapalestina. Tupo katika nyakati zilizosheni midahalo kila kona. Tutarejea vipi kwenye uhalisia?
Nimekuwepo Afrika Kusini na kuishi humo miaka 22 ya utu uzima wangu. Ubaguzi wa rangi ulidumu kwa kipindi kirefu na taifa hilo likajipa fursa ya kuanza upya kupitia mazungumzo ya kukiri maovu yaliyofanyika na kuumiza watu wengi. Hata mwenye kufanya dhuluma alikuwa amepoteza utu wake wakati akimdhulumu mdhulumiwa.
Hili lilipelea kila mtu kujikusanya na kuzingatia umuhimu wa kukubali ya kuwa maovu ya yalikuwepo huku umuhimu wa amani na ushirikiano ukipigiwa upato. Siasa za ukweli na ushirikiano ndiyo njia pekee.