Wapalestina wametumia mitandao ya kijamii kuonyesha ukatili wa vita vya mauaji ya Israeli dhidi ya watu wake, na kuruhusu ulimwengu kushuhudia huku vyombo vya habari vya kawaida vikisita kuripoti ukatili huo. (Reuters/Saleh Salem)

Na Dk. Sahar Khamis / Felicity Dogbatse

Vita dhidi ya Gaza vilivyozuka mwezi Oktoba vimeteka hisia za kimataifa kutokana na hasara kubwa ya kibinadamu, uharibifu mkubwa wa miundombinu, na idadi kubwa ya majeruhi. Kwa mujibu wa UNICEF, makumi ya maelfu ya watu wameuawa katika kipindi cha miezi 10, wakiwemo zaidi ya watoto 15,000.

Wengi zaidi wamejeruhiwa vibaya au hawajulikani waliko chini ya vifusi, na mamia ya maelfu wameyahama makazi yao, wakitafuta hifadhi katika makao yaliyojaa watu, yasiyo na usafi. Hasara ya kiuchumi imekuwa mkubwa vile vile, na kufikia mabilioni ya dola, ikidhoofisha zaidi uchumi wa Gaza ambao tayari unayumbayumba.

Ulimwengu umejibu vipi? Hebu tuangalie kwa karibu vyombo vya habari vya kimataifa vimeangazia vipi vita hivi, tukilinganisha vyombo vya habari vya Magharibi na kile kinachoangaziwa kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Vikwazo vyenye matatizo

Utangazaji wa vita vya Gaza katika vyombo vya habari vya Magharibi umekuwa wa shida kwa sababu kadhaa.

Kulingana na ukaguzi wa Taasisi ya Al Jazeera mnamo Januari, mambo mengi kama vile taratibu za vyombo vya habari, sera za shirika, na mifumo ya kijamii imeathiri uandishi wa habari wa vita hivi, na kuathiri kina na ubora wa simulizi.

Taratibu za vyombo vya habari, ambazo zinajumuisha mazoea ya kawaida na mtiririko wa kazi ndani ya mashirika ya habari, mara nyingi hutanguliza kasi na ufanisi badala ya kuripoti kwa kina. Sera za shirika, kama vile miongozo ya uhariri na ugawaji wa rasilimali, huwabana zaidi wanahabari, jambo linaloweza kusababisha utangazaji kuwa duni.

Mrundiko huu wa athari husababisha kutayarishwa kwa ripoti ambayo inaweza kukosa kina na ubora unaohitajika ili kuwasilisha kikamilifu utata wa mzozo, na hivyo kuathiri uelewa wa umma na mazungumzo.

Vyombo vya habari vya kawaida vimekabiliwa na vikwazo kuhusiana na utendakazi wake Gaza, ikiwa ni pamoja na vikwazo vya kisiasa, changamoto za kiitikadi na vikwazo vya vifaa.

Vyombo vya habari vya Magharibi vimekosolewa kwa kushindwa kuripoti juu ya mgogoro wa Gaza kwa usahihi, haki, na kwa kina.

Ukosoaji mmoja mkubwa ni uandishi wa upendeleo ambao mara nyingi huweka kipaumbele simulizi la Israeli juu ya simulizi la Palestina, likitegemea sana ripoti rasmi kutoka upande wa Israeli bila kuangalia ukweli wa kutosha.

Zaidi ya hayo, kuna ukosefu wa muktadha wa kutosha wa kihistoria na ubinadamu wa wahasiriwa wa Palestina, mara nyingi hupuuza mateso yao ya kila siku.

Zaidi ya hayo, ufikiaji mdogo wa waandishi wa habari wa kimataifa kwenda Gaza kwa sababu ya vizuizi vya kisiasa kutoka kwa upande wa Israeli na wasiwasi wa usalama unazuia zaidi kuripoti kwa kina.

Hii inapelekea vyombo vingi vya habari vya kimataifa kutegemea taarifa rasmi za kiserikali na waandishi wa habari wanaofatwana na wanajeshi, na hivyo kuzuia utofauti wa mitazamo na kina cha uandishi wa habari.

Matatizo ya mzozo wa Gaza mara nyingi unafanywa kana kwamba ni "mgogoro wa Israeli na Hamas," unaozidisha upunguzaji na uondoaji wa muktadha wa utangazaji wa vyombo vya habari vya vita.

Kulingana na uchanganuzi wa Intercept mnamo Januari, CNN, MSNBC, na FOX News zote zilitoa ripoti potofu wakati wa miezi ya kwanza ya vita vya Gaza. Vyombo vikubwa vya habari kama vile New York Times, Washington Post na Los Angeles Times vilipendelea upande wa Israeli, vikionyesha upendeleo thabiti dhidi ya Wapalestina na kutozingatia mateso yao ya kila siku.

Utangazaji wa vyombo vya habari vya Magharibi, hasa vyombo vya habari vya Marekani, ulifichua mapungufu kadhaa. Hizi ni pamoja na kuripotiwa kwa hali ya duni majeruhi wa kiraia wa Palestina, ukosefu wa simulizi za kina kuhusu taarifa za kibinafsi za hasara na mateso, na uwakilishi usiofaa wa mitazamo ya Wapalestina.

Mitandao ya kijamii inang'aa

Kinyume chake, mitandao ya kijamii imejaza pengo katika kuripoti vita vya Gaza. Katika miaka ya hivi karibuni, imeibuka kama nguvu kubwa katika kuunda simulizi kuhusu migogoro ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na hii ya hivi karibuni.

Majukwaa ya mitandao ya kijamii yamekuwa nyenzo muhimu kwa kutoa simulizi mbadala. Majukwaa kama vile Instagram, Facebook, na Twitter inatoa sauti kwa watu wa kila siku mashinani, ikionyesha hadithi zao za kibinafsi, picha na masasisho ya wakati halisi.

Machapisho na heshtegi, kama vile #freepalestine na #Gazaunderattack, zimeongeza uhamasishaji na kuchochea mazungumzo yanayopita mipaka ya kijiografia na kiitikadi.

Uandishi wa habari wa kiraia kwenye mitandao ya kijamii umewezesha mitazamo tofauti kwa kuwasilisha simulizi ambazo huenda zisipatikane kwenye vyombo vya habari vya kawaida. Uwekaji demokrasia huu wa habari huruhusu raia wa kawaida kushiriki mitazamo yao na hadhira pana ya kimataifa.

Mitandao ya kijamii pia imetoa majukwaa kwa wanaharakati, waandishi wa habari, na umma ili kuvutia watu kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na masuala ya kibinadamu ambayo mara nyingi hupuuzwa na vyombo vya habari vya kawaida.

Mitandao ya kijamii huathiri kwa kiasi kikubwa maoni ya umma na kushiriki simulizi kuhusu vita vya Gaza. Kwa mfano, "mitandao ya kijamii huathiri jinsi Wamarekani, hasa vijana wa Marekani, wanavyochukulia mzozo huo.

Watazamaji wachanga zaidi wanapata habari zao kutoka kwa mitandao ya kijamii-hasa TikTok na Instagram-kuliko kutoka kwa vyombo vya habari vya kawaida, kama vile magazeti na televisheni."

Kampeni za mtandaoni huongeza uhamasishaji na kuhimiza hatua za kimataifa, kama vile uchangishaji fedha, kwa kutumia taswira za sauti na heshtegi kama vile #GazaUnderAttack.

Zaidi ya hayo, majukwaa ya mitandao ya kijamii huwezesha masasisho ya wakati halisi na kutoa jukwaa la mitazamo tofauti. Kwa mfano, Rosie na @ajplus kwenye TikTok hutoa ripoti za moja kwa moja kuhusu Gaza, huku @mizna_arabart na e7saswafa wakitumia Instagram kuripoti matukio na majeruhi kutoka pande zote mbili.

Majukwaa haya huwezesha watu kuona zaidi ya yale ambayo vyombo vya habari vya utangazaji hutoa.

Upanga wenye ncha mbili

Ingawa mitandao ya kijamii inatoa fursa nzuri kwa simulizi mbadala kuhusu vita vya Gaza, pia ina mapungufu na vikwazo. Kuongezeka kwa ubaguzi ni mojawapo ya vikwazo hivyo, kwani majukwaa ya mitandao ya kijamii kupitia mifumo ya algorithimi yanaweza kukuonyehsa taarifa zinazoimarisha imani zao.

Usambazaji wa haraka wa habari potofu, na propaganda huleta changamoto nyingine kubwa, inayolazimu ujuzi muhimu wa kusoma na kuandika wa vyombo vya habari kwa watumiaji wa mtandaoni.

Zaidi ya hayo, matumizi ya mitandao ya kijamii katika maeneo yenye matatizo yanaleta maswali ya kimaadili kuhusu usalama na faragha. Taarifa nyeti zinazotolewa kwa umma zinaweza kuwaweka wale walioko mashinani katika hatari.

Kwa mfano, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ilibidi itoe tamko la kukanusha habari zenye madhara na za uwongo kama jibu kwa habari za uwongo ambazo zilisambaa mitandaoni kuhusu kazi yao Israeli na Palestina.

Licha ya mapungufu haya, mitandao ya kijamii inasalia kuwa muhimu kwa ajili ya kuongeza ufahamu, kuimarisha uhamasishaji na mshikamano, na kushawishi utangazaji wa vyombo vya habari vya kawaida. Mitandao ya kijamii hutoa masasisho ya wakati halisi, majukwaa ya mitazamo mbalimbali, na kutoa fursa kwa akaunti za mashahidi, kujaza mapengo katika utangazaji wa kawaida wa vyombo vya habari. Kwa kufanya hivyo, majukwaa yanakuza sauti ambazo mara nyingi hazijasikika au kupuuzwa katika vyombo vya habari vya jadi, kutoa uelewa wa kina zaidi wa matukio ya sasa.

Licha ya mapungufu haya, mitandao ya kijamii inasalia kuwa muhimu kwa ajili ya kuongeza ufahamu, kuimarisha uhamasishaji na mshikamano, na kushawishi utangazaji wa vyombo vya habari vya kawaida.

Mitandao ya kijamii hutoa masasisho ya wakati halisi, majukwaa ya mitazamo mbalimbali, na kutoa fursa kwa kurasa za mashahidi walioko mashinani, kujaza mapengo katika utangazaji wa kawaida wa vyombo vya habari.

Kwa kufanya hivyo, majukwaa yanakuza sauti ambazo mara nyingi hazijasikika au kupuuzwa katika vyombo vya habari vya kawaida, kutoa uelewa wa kina zaidi wa matukio ya sasa.

Utangazaji wa vyombo vya habari vya Magharibi kuhusu vita vya Gaza mara nyingi umeimarisha upendeleo kwa kutowakilisha mitazamo ya Wapalestina na kuacha muktadha wa kihistoria, na hivyo kuchagiza maoni ya umma katika mchakato huo.

Majukwaa ya media ya kijamii kama Instagram na TikTok husaidia kujaza mapengo haya kwa kutoa vyanzo vya haraka kutoka kwa wale walioathiriwa, lakini pia huanzisha hatari kama vile habari potofu na vitisho vya usalama. Ujuzi wa vyombo vya habari ni muhimu ili kukabiliana na changamoto hizi na kutumia manufaa ya mitandao ya kijamii wakati wa migogoro.

Waandishi

Dk. Sahar Khamis ni mtaalamu wa vyombo vya habari vya Kiarabu na Kiislamu, mwenye taaluma na uzeofu mkubwa. Aliwahi kuwa Mkuu wa Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Qatar na alikuwa profesa mgeni katika Chuo Kikuu cha Chicago. Dk. Khamis pia ni mchambuzi wa vyombo vya habari, mzungumzaji wa umma, na kamishna wa haki za binadamu huko Maryland.

Felicity Sena Dogbatse yuko katika mwaka wake wa pili wa Ph.D. ni mwanafunzi wa Rhetoric & Political Culture katika Idara ya Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Maryland.

Kanusho: Maoni yaliyotolewa na mwandishi hayawakilishi lazima maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.

TRT Afrika