Nchini Uingereza, mfalme ndiye mkuu wa nchi/ Picha: Reuters

Takriban viongozi 12 kutoka Afrika walihudhuria sherehe ya kutawazwa kwa Mfalme Charles III katika ukumbi wa Westminster Abbey mjini London, Uingereza siku ya Jumamosi. Wengi wao walikuwa kutoka mataifa ya Jumuiya ya Madola.

Viongozi hao mashuhuri wa serikali mbalimbali wa nchi za Africa ni pamoja na William Ruto wa Kenya, Rais Paul Kagame wa Rwanda, George Weah wa Liberia, Lazarus Chakwera wa Malawi, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na Hakainde Hichilema wa Zambia.

Wengine walikuwa Mfalme Mswati III wa Eswatini, Rais Mohamed Bazoum wa Niger, Faure Gnassingbe wa Togo na Ali Bongo Ondimba wa Gabon.

Rais wa Cameroon Paul Biya alimtuma Waziri Mkuu wa taifa hilo Joseph Dion Ngute kumwakilisha katika kutawazwa kwa Mfalme.

Mfalme Charles III alikula Kiapo cha Kutawazwa na akawa mfalme wa kwanza kuomba kwa sauti wakati wa kutawazwa kwake 

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara pia alikabidhi mwaliko huo kwa makamu wake, Tiémoko Meyliet Koné.

Kando na viongozi wa Afrika, kutawazwa kwa Mfalme Charles III kulihudhuriwa na mamia ya wageni mashuhuri akiwemo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese, Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula Von der Leyen na mke wa rais wa Marekani Jill Biden.

Mfalme nchini uingereza pia anaongoza mikutano ya kila mwezi ya Baraza la Faragha, ili kuidhinisha Maagizo katika Baraza. Picha/Reuters

Rais Macron alitweet Jumamosi: "Hongera kwa Mfalme Charles III na Malkia Camilla, marafiki wa Ufaransa. Najivunia kuwa pamoja nawe katika siku hii ya kihistoria.”

Jill Biden, ambaye alimwakilisha Rais Joe Biden, alisema kwenye Twitter: "Marekani na Uingereza zina uhusiano muhimu sana. Ni heshima kuiwakilisha Marekani katika siku hii ya kihistoria huko Westminster Abbey."

Katika ujumbe wake, Rais Biden alisema: "Hongera kwa Mfalme Charles III na Malkia Camilla kwa kutawazwa kwao. Urafiki wa kudumu kati ya U.S. na U.K. ni chanzo cha nguvu kwa watu wetu wote wawili.

Rais Ruto wa Kenya naye alisema kwenye Twitter kwamba nchi yake "inathamini uhusiano mzuri inaofurahia na Uingereza."

Rais Hichilema wa Zambia alisema anajivunia "kushuhudia tukio hili la kihistoria, ambalo lilifanyika mara ya mwisho miaka 70 iliyopita".

Samia Suluhu, Rais wa Tanzania, ambayo pia ni taifa la Jumuiya ya Madola, alisema kwenye Twitter: “Pongezi za dhati kwa Mfalme Charles III na Malkia Camilla kwa kutawazwa kwako. Utawala wako na ujazwe na amani, utulivu na mafanikio. Ninatazamia kuinua uhusiano thabiti na wa kihistoria wa Tanzania na Uingereza kwa kiwango cha juu zaidi. Rais Suluhu hakuhudhuria sherehe ya utawazaji.

Mfalme Charles, 74, alikua Mfalme kufuatia kifo cha mama yake, Malkia Elizabeth II, mnamo Septemba 8, 2022, kutawazwa kwake Jumamosi kulikuwa kutawazwa rasmi kwa mfalme.

Mfalme nchini uingereza ana uwezo kuteua kama vile majaji wakuu chini ya ushauri wa serikali.Picha/Reuters.

Mfalme Charles III alikula kiapo cha kutawazwa na akawa mfalme wa kwanza kuomba kwa sauti wakati wa kutawazwa kwake. Katika sala yake, aliomba “kuwa baraka” kwa watu wa “kila imani na usadikisho.”

Mara tu Mfalme alipotawazwa, mkewe, Malkia Camilla, 75, alitawazwa katika hafla fupi. Sherehe za Mei 6 zilikuwa za kwanza nchini Uingereza tangu kutawazwa kwa Malkia Elizabeth II mnamo 1953.

Nchini uingereza mfalme ana uwezo wa kupokea mabalozi wanaoingia na kutoka uingereza.Picha Reuters.

Nchini Uingereza, mfalme ndiye mkuu wa nchi. Mfalme pia anaongoza mikutano ya kila mwezi ya Baraza la Faragha, ili kuidhinisha maagizo katika Baraza; inapokea mabalozi wanaoingia na kutoka; hufanya uteuzi mwingine mwingi, kama vile majaji wakuu, lakini katika haya yote anafanya kazi kwa ushauri wa serikali.

TRT Afrika