Bunge ya Uingereza umepitisha Mswada wa Uhamiaji Haramu. Unapendekeza kuondoa hifadhi kwa mtu yeyote anayefika kwa njia "isiyo ya kawaida" nchini Uingereza.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa zinasema mswada huu unawazuia kuwasilisha ulinzi wa wakimbizi au madai mengine ya haki za binadamu, bila kujali jinsi hali zao zinavyolazimisha.
"Kwa miongo kadhaa, Uingereza imetoa kimbilio kwa wale wanaohitaji, kulingana na majukumu yake ya kimataifa - mila ambayo imekuwa ya kujivunia." amesema mkuu wa Grandi. Sheria hii mpya inapunguza kwa kiasi kikubwa mfumo wa kisheria ambao umewalinda wengi, na kuwaweka wakimbizi kwenye hatari kubwa katika uvunjaji wa sheria za kimataifa,” Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi alisema.
"Muswada huo pia unasema kwa kuongeza, inahitaji kuondolewa kwao hadi nchi nyingine, bila hakikisho kwamba wataweza kupata ulinzi huko. Inaunda mamlaka mpya ya kizuizini, na uangalizi mdogo wa mahakama," mashirika hayo mawili yamesema katika taarifa ya pamoja.
Wahamiaji kupelekwa Rwanda
Mswada huu ukipitishwa kuwa sheria inamaanisha kuwa watu watakaoingia Uingereza kinyume cha sheria watarejeshwa katika nchi yao au kuhamishiwa Rwanda.
Rwanda na Uingereza zilifanya makubaliano ya kuwa Rwanda itapokea wahamiaji wanaokimbilia Uingereza. Uingereza ulisema mpango huo utazuia watu wanaowasili nchini Uingereza kupitia "njia zisizo halali, au njia hatari, kuingia Uingereza.
Rwanda ingepokea takriban dola milioni 177 ili kupokea wahamiaji wanaoingia Uingereza.
Lakini Juni mwaka huu mahakama kuu nchini Uingereza ulitupilia mbali pendekezo hili na kusema kwamba iko kinyume na sheria.
Ilidai kuwa Rwanda haiwezi kuchukuliwa kama nchi ya tatu kwa wakimbizi yenye usalama. Pia ilidai kuwa kuna hatari ya wakimbizi wanaopelekwa Rwanda kurejeshwa katika nchi zao wanapotoroka na kukabiliwa na mateso au kutendewa ukatili.
Inaripotiwa kuwa mwaka wa 2022, watu 45,755 walikuja Uingereza kwa boti ndogo hasa kutoka Ufaransa. Zaidi ya 11,000 wamewasili mwaka huu.
Serikaii ya Rwanda imesisistiza kuwa iko na usalama wa kutosha kwa wahamiaji.
"Rwanda ni mojawapo ya nchi salama zaidi duniani na tumetambuliwa na shirika la kutetea haki za wakimbizi, UNHCR na taasisi nyingine za kimataifa kwa jinsi tunavyowalinda wakimbizi," msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo alisema.
" Inawazuia kuwasilisha ulinzi wa wakimbizi au madai mengine ya haki za binadamu, bila kujali jinsi hali zao zinavyolazimisha. Kwa kuongeza, inahitaji kuondolewa kwao hadi nchi nyingine, bila hakikisho kwamba wataweza kupata ulinzi huko. Inaunda mamlaka mpya ya kizuizini, na uangalizi mdogo wa mahakama," imeongezea