Mkutano wa G77 na China kuhusu sayansi, Teknolojia na Maendeleo, umeanza. Mkuu wa UN Antonio Guterres anahudhuria / Picha: AFP

Viongozi na Wakuu wa nchi na serikali 30 kutoka Afrika, Asia na Marekani ya kusini wamekongamana kwa mkutano wa siku mbili mjini Havana. China imewakilishwa na afisa mkuu wa Chama Cha Kikomunisti Li Xi.

Miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria ni Rais Luiz Inacio Lula Da Silva Wa Brazil, Gustavo Petro wa Colombia na Alberto Fernandez wa Argentina.

Viongozi wa Afrika wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Rais wa Angola Joao Lourenco, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.

Rais wa Uganda Paul Kagame afanyiwa gwaride la heshima baada ya kutua Havana, CUBA. Picha: Ikulu ya Rwanda

Wengine ni pamoja na Makamu wa Rais wa Nigeria Kashim Shettima, Makamu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua, Makamu wa Rais wa Uganda Jessica Alupo na Makamu wa Rais wa Zimbabwe Constantino Chiwenga, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Demeke Mekonnen miongoni mwa wengine.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ambaye aliwasili katika kisiwa hicho alhamisi, anashiriki mkutano huo.

Guterres, atatoa hotuba ya ufunguzi pamoja na Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel, baada ya hivi karibuni kuhudhuria mikutano wa kilele wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na mkutano wa G20 jijini Delhi nchini India pamoja na kundi la BRICS ambalo linajumuisha Urusi.

Mkuu wa UN Antonio Guterres, amewasili katika kisiwa hicho alhamisi, kushiriki mkutano huo wa G77+China. Picha: Reuters

Kabla ya mkutano huo wa Havana, Guterres alisema " huu wingi wa mikutano ya kilele inaashiria kuongezeka kwa wingi wa ulimwengu wetu."

Aidha, ameonya kwamba " mgawanyiko unaweza kuwa sababu ya kuongezeka kwa mvutano wa kijiografia, na matokeo mabaya."

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kumalizika Jumamosi kwa taarifa inayosisitiza " haki ya maendeleo katika utaratibu wa kimataifa unaozidi kuwa wa kipekee, sio na usawa, usio wa haki na wa kupora," Waziri wa Mambo ya Nje wa cuba, Bruno Rodriguez, aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatano.

Dukuduku za taarifa ya awali kulingana na makubaliano ya mwisho, inasisitiza vikwazo vingi vinavyokabili mataifa yanayoendelea, na inajumuisha "wito wa kubuniwa kwa mfumo mpya wa kiuchumi ulimwenguni", alisema.

Muungano huo ulianzishwa mnamo 1964 na nchi 77 za kusini mwa dunia "kuelezea na kutetea maslahi yao ya pamoja ya kiuchumi na kuongeza uwezo wao wa mazungumzo ya pamoja", kulingana na tovuti ya kundi hilo.

Nitazingatia kurudisha Ajenda ya 2030," akimaanisha orodha ya malengo ya UN kumaliza umaskini na njaa na kuvunja mabadiliko ya hali ya hewa, kati ya zingine.

Antonio Guterres

Imefikia wanachama 134, mpaka sasa ikiwemo China iliyoorodheshwa na tovuti hiyo ingawa China inasema sio mwanachama kamili.

Cuba ilichukua Urais wa mzunguko wa muungano huo mwezi Januari.

Uwepo wa viongozi wa dunia katika ardhi ya Cuba ni sawa na "kutambuliwa kwa serikali ya Cuba" hata kama nchi hiyo inapambana na changamoto zake mbaya zaidi za kiuchumi ndani ya miongo mitatu, mchambuzi aliiambia AFP.

"Licha ya kushuhudiwa wakati mgumu, Cuba imetambuliwa kama mpatanishi halali," Mtaalamu wa uhusiano wa kimataifa wa Cuba Arturo Lopez-Levy, Profesa katika Chuo kikuu Cha Autonomous Cha Madrid.

Kisiwa hicho kinachotawaliwa na wakomunisti bado kiko chini ya vikwazo vilivyowekewa na Marekani tangu 1962.

Katika miezi ya hivi karibuni, Diaz-Canel ameiwakilisha G77+China katika mikutano kadhaa ya kimataifa ikiwa ni pamoja na mkutano wa kilele wa fedha duniani, ulifanyika huko Paris mwezi Juni na mkutano wa EU na mataifa ya Amerika Kusini na Karibea mwezi Julai.

Kauli mbiu ya mkutano wa Havana ni jukumu la" sayansi, teknolojia na uvumbuzi " katika maendeleo.

AFP