Israel imekuwa ikitumia "silaha zisizo za kawaida" zinazosababisha moto mkali kwa miili ya waathirika, Wizara ya Afya ya Gaza imesema.
Kulingana na msemaji wa Wizara hiyo, Ashraf Al Qudra kupitia taarifa iliyotolewa, " wahudumu wa afya walifuatilia matumizi ya silaha zisizo za kawaida zilizosababisha kuchoma miili ya waathirika na waliojeruhiwa.”
Israeli haijatoa tamko lolote kufikia sasa juu ya taarifa hizo.
Katika taarifa tofauti, Al Qudra alionya kuhusu "hatari kubwa " ambayo inaweza kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000 na wagonjwa wa figo zilizofeli hivyo kusababisha vifo zaidi. Hali inaweza kuwa mbaya zaidi iwapo usambazaji wa mafuta hautafanyika kwa wakati katika hospitali na sekta nzima ya huduma za afya.
"Kushindwa kufikisha mafuta katika hospitali kutasababisha athari kubwa ambayo itasababisha vifo vya wagonjwa 1,100 wa figo zilizoshindwa kufanya kazi, wakiwemo watoto 38," alisema.
Aidha, ametoa wito kwa raia ambao " wana kiasi chochote cha mafuta aina ya dizeli kuchangia mafuta haraka katika hospitali ili kuokoa maisha ya waliojeruhiwa na wagonjwa."
Moshi mkubwa ulizidi kutanda baada ya ndege za kivita za Israel kushambulia eneo la Rafah, Gaza, mnamo Oktoba 22, 2023.
Kuongezeka kwa idadi ya vifo
kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza, Wapalestina 4,651, wakiwemo watoto 1,873 na wanawake 1,023 wameuawa huku watu 14,245 wakijeruhiwa vibaya baada ya jeshi la Israel kuendelea kuilenga Gaza kwa mashambulizi makali ya anga ambayo yameharibu vitongoji vyote vya eneo hilo.
Idadi ya watu wasiyojulikana wamenaswa chini ya vifusi
Mzozo wa Gaza, ambao umekuwa chini ya mabomu ya Israeli na kuzingirwa kabisa tangu Oktoba 7, ulianza wakati kundi la Palestina la Hamas lilipoanzisha 'Operesheni ya Mafuriko ya Al Aqsa,' shambulio la mshangao lenye pande nyingi ambalo lilijumuisha mlipuko wa uzinduzi wa roketi na uingiliaji ndani ya Israeli kupitia ardhini, baharini na kwa njia ya anga.
Katika taarifa yao, Hamas ilisema kuwa, uvamizi huo ulikuwa ni kulipiza kisasi kwa uvamizi wa msikiti wa Al Aqsa na kuongezeka kwa vurugu za wahamiaji wa Israeli dhidi ya Wapalestina.
Kwa upande wake, jeshi la Israeli kisha lilizindua 'Operesheni ya Mapanga ya Chuma' huko Gaza.
Zaidi ya Waisraeli 1,400 wameuawa katika vita hivyo.