Ndege wanaruka juu ya Nablus katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israeli jua likizama mnamo Septemba 9, 2024. / Picha: AFP

Na

Ahmad Ibsais

Mauaji ya wiki hii ya Al Mawasi, ambayo yalishuhudia silaha za maangamizi zikitumiwa dhidi ya wakimbizi waliokuwa wamejificha kwenye mahema, ni uthibitisho wa ukweli kwamba ulimwengu unazidi kuzoea umwagaji damu wa Wapalestina. Na haifanyi chochote kuizuia.

Tangu tarehe 7 Oktoba, tumesikia kuhusu "haki ya kujilinda" ya Israeli inayoonekana kutokuwa na kikomo. Kuna njia mbili za kuangalia hili. Ikiwa tutakubali kuwa ni kweli, basi lazima tukubali kwamba Wapalestina wana haki hiyo pia - hasa katika kukabiliana na mauaji mengi ambayo yamefanyika katika mwaka uliopita.

Na ikiwa hatutakubali kuwa ni kweli, basi Wapalestina pekee ndio wenye haki isiyoisha ya kujilinda katika harakati zao za ukombozi zinazoendelea. Hata hivyo, katika vyombo vya habari vya Magharibi na siasa, "haki" hii daima inaonekana kuwa ya masharti linapokuja suala la wahasiriwa wa ubeberu.

Kwa miaka mingi, maneno kama "Mhimili wa Uovu" yamekuwa yakitumiwa kama zana ya propaganda ili kuweka mataifa na watu wote kama vyanzo vya vitisho visivyoweza kuzuiwa. Lakini ndani ya Palestina, ambapo ukaidi umekua kwa kasi kwa vizazi kadhaa, ukweli hauwezi kuwa tofauti zaidi.

Kambi za wakimbizi huko Nablus, Jenin, na Tulkarem sio vituo vya ugaidi au uovu. Ndio chimbuko la upinzani wetu—mfano ulio hai wa roho ya kudumu kwa taifa la Palestina, ambayo inakataa kuvunjwa na miongo kadhaa ya kukaliwa kwa mabavu, kunyimwa haki za msingi, na kuzingirwa.

Wakati mtazamo wa ulimwengu mara nyingi ukilenga Gaza kama ishara ya ukaidi, Israeli imeshindwa kuitiisha na kuiweka chini ya udhibiti licha ya kampeni za kijeshi zisizo na kikomo.

Hivi sasa, mpango wa Wazayuni umeelekezwa kwenye Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ukilenga kambi za wakimbizi za Jenin, na kuharibu asilimia 80 ya mitaa ya mji huo, ambapo wakazi wamejikita katika harakati za ukombozi tangu kuundwa kwao.

Kambi hizi, zilizokabiliwa na maafa ya kuhama, zimebadilika na kuwa ngome za umoja na ukaidi.

Kambi kama mahali pa kuzaliwa kwa ukaidi

Kambi za wakimbizi katika Ukingo wa Magharibi, haswa huko Nablus, Jenin, na Tulkarem, sio tu mahali ambapo waliohamishwa wanaishi. Bali ni chimbuko la ukaidi na umoja wa Wapalestina, ambayo inaendelea kupinga ukoloni na unyanyasaji.

Kihistoria, kambi hizi zimetumika kama vituo vya kuandaa siasa na elimu, licha ya majaribio ya Israeli kuwadhalilisha wenyeji wao kwa kuyatambua kama maeneo yenye itikadi kali.

Nablus, Jenin, na Tulkarem yana historia ndefu ya ukaidi mkali tangu Intifada ya Kwanza mwaka wa 1987. Haya ndiyo maeneo ambayo maandamano dhidi ya uvamizi wa Israeli yalipangwa, ambapo vijana walijifunza kukaidi hata walipokabiliwa na dhuluma kali zaidi.

Kuzingirwa na kuharibiwa kwa kambi ya wakimbizi ya Jenin mwaka 2002, wakati wa Intifadha ya Pili, inasalia kuwa mojawapo ya sura za kikatili zaidi katika historia ya upinzani ya Ukingo wa Magharibi.

Hata hivyo, hata katikati ya vurugu hizo, kambi hiyo haikushindwa kamwe. Watu walivumilia, wakajenga upya, na wakaendelea kukaidi.

Haki ya kujilinda

Leo, katika hali ya uhalifu wa kivita uliodhahiri, utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden umesema uungaji mkono wake usioyumba kwa Israeli, na kuitaja uhalifu wa Israeli dhidi ya Wapalestina kama "haki ya kujilinda."

Hapa ndipo tunapaswa kuwa waangalifu. Wazayuni na vyombo vya habari vya Magharibi vinaainisha upinzani wa silaha wa Wapalestina kama vitendo vya "ugaidi" au "misimamo mikali." Hata hivyo vitendo dhidi ya utawala wa Kizayuni si chochote.

Ukaidi na kujitawala ni haki zetu zisizoweza kuondolewa na zilizowekwa. Masimulizi yanaanza na ukweli kwamba kabla ya Israeli, kulikuwa na watu huko. Kwa mujibu wa ukweli huu, hakuna kitu kinachoitwa "kujilinda kwa Israeli," kwani ukweli wa ukweli huu unawafanya moja kwa moja kuwa wachokozi na kuwapa Wapalestina haki ya kupinga kwa njia yoyote.

Kulingana na Kifungu cha 42 cha Kanuni za Hague za 1907, "eneo huwa linakaliwa kwa mabavu pale linapowekwa chini ya mamlaka ya jeshi lenye uadui."

Hata hivyo, linapokuja suala la Palestina hili ghafla linakuwa gumu sana kulielewa. Tangu 1948, Palestina imekuwa ikikaliwa kwa mabavu na taifa la kikoloni linalozidi kupanuka. Palestina haina jeshi na Wapalestina hawana haki ya kuhama. Hivyo wanachukuliwa kuwa "Watu Waliolindwa" chini ya Umoja wa Mataifa ambayo inafafanua maana wazi ya ukaliaji wa mabavu.

Vitendo vya kinyama vinavyofanywa na ukandamizaji na utawala wa kitaasisi wa Wapalestina (kukamatwa kiholela, kuwaangamiza, kuhamisha idadi ya watu, n.k.) vinatupa haki ya kimaadili na kisheria wa kukaidi kutumia silaha.

Mwaka 1982, Azimio nambari 37/43 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliidhinisha, bila shaka, "haki isiyoweza kuepukika" ya watu wa Palestina ya "kujitawala, uhuru wa kitaifa, mamlaka kamili, na uhuru bila ya uingiliaji kati wa kutoka nje."

Zaidi ya hayo, azimio hilohilo linathibitisha tena uhalali wa kisheria wa watu wa Palestina na mapambano yetu ya haki hizo kwa "njia zote zilizopo, ikiwa ni pamoja na mapambano ya silaha."

Ingawa kiwango cha mapambano ya silaha hakijatajwa, viwango vya kimataifa vinachukulia kwamba kinashughulikia kiwango hadi ukombozi ufikiwe. Ni haki ya msingi ya binadamu ya Wapalestina kupinga kuuawa.

Mwanzo mpya

Ukaidi tunaoshuhudia leo ni tofauti na ya awali kwa njia tofauti. Ingawa nyakati za awali za ukaidi mara nyingi uligawanyika, huku mirengo tofauti ikifuata mikakati yao, hivi leo kuna umoja mkubwa kati ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Makundi tofauti ya kisiasa, ambayo hapo awali yangeweza kufanya kazi tofauti, sasa yanafanya kazi pamoja kwa njia ambazo hazijawahi kushuhudiwa.

Katika eneo la Nablus, kwa mfano, vikundi vya upinzani vya ndani vimejitokeza, vinavyojumuisha watu kutoka kwa makundi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Fatah, Hamas, na Jihadi ya Kiislamu. Wameunda mfumo uliopangwa, wa ushirika ili kupambana na uvamizi wa Israeli.

Ushirikiano huu ni jibu la moja kwa moja kwa uchokozi unaozidi wa Israeli, lakini pia unachochewa na hali inayokua ya madhumuni ya pamoja katika jamii ya Wapalestina.

Mbinu za Israeli katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu ni sawa na zile ambazo zimetumia huko Gaza. Kuzingira, ubomoaji wa nyumba, mauaji yaliyolengwa ya viongozi wa upinzani-hizi ni mbinu za ukaliaji wa mabavu ambazo zimetumiwa kwa miongo kadhaa.

Na bado, kama vile hatua hizi zimeshindwa huko Gaza, zinaelekea kushindwa katika Ukingo wa Magharibi. Ustahimilivu wa watu katika Ukingo wa Magharibi, hasa katika kambi za wakimbizi, unatokana na uhusiano wao wa kina na ardhi na historia yao ya ukaidi.

Licha ya juhudi za kufuta uwepo wa Wapalestina, ni katika maeneo kama vile Jenin na Nablus ambapo utambulisho huu umehifadhiwa kwa ukali zaidi.

Kama vile Mahmoud Darwish amesema "Tunalo hapa duniani linalofanya maisha kuwa ya thamani."

Zaidi ya hayo, jumuiya ya kimataifa, licha ya kushindwa kwake, imekua ikifahamu zaidi dhuluma inayofanywa. Upinzani wa Wapalestina hauonekani tena kuwa wabila maana.

Ni sehemu ya harakati ya kimataifa ya haki na haki za binadamu, na masaibu ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu yanazidi kuzingatiwa kwa njia ambazo Israeli haiwezi kudhibiti.

Nguvu ya muqawama wa Wapalestina iko katika uwezo wake wa kukusanyika sio tu uwanjani, bali ni ya kuvuka mipaka na kupitia mshikamano wa watu kila mahali wanaoamini katika haki ya kujitawala.

Mwishoni, Israeli itafeli katika Ukingo wa Magharibi kwa sababu zile zile ambazo imeshindwa huko Gaza.

Ukaliaji wa mabavu hata uwe wa kikatili kiasi gani, haiwezi kufuta mapenzi ya watu walioazimia kuwa huru.

Kambi za wakimbizi huko Nablus, Jenin, na Tulkarem sio tu sehemu ya jamii ya Wapalestina—ndio kiini chake. Na kutokana na machimbuko haya ya ukaidi, mapambano yataendelea hadi pale Palestina itakapokuwa huru.

Mwandishi, Ahmad Ibsais ni Mpalestina wa kizazi cha kwanza aliyezaliwa Marekani na mwanafunzi wa sheria ambaye anaandika jarida la State of Siege.

TRT Afrika