Austria ilirekodi idadi kubwa zaidi ya kesi zinazohusiana na chuki dhidi ya Waislamu mwaka jana, tangu ilipoanza kuweka rekodi mwaka 2015, ripoti ilisema.
Ripoti ya kila mwaka ya Kituo cha Nyaraka cha kuangazia chuki na ubaguzi dhidi ya Waislamu, iliyotolewa Jumatatu, ilichapishwa kwenye tovuti yake.
Ilisema idadi ya kesi zilizoripotiwa imeongezeka, haswa tangu kuzuka kwa vita vya Israeli dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7 mwaka jana.
Kesi zaidi zilirekodiwa kutoka Oktoba hadi Disemba kuliko katika miezi tisa ya kwanza ya 2023.
Mahali pa kwanza ambapo kesi zaidi ziliripotiwa kutoka Oktoba ilikuwa shule, ripoti hiyo ilisema. Katika sekta ya elimu, kesi za chuki dhidi ya Uislamu ziliripotiwa na wazazi, wanafunzi na walimu.
Kwa ujumla, 66.7% ya kesi zilizorekodiwa zilifanyika mtandaoni na 33.7% nje ya mtandao. Takriban 87.8% ya matukio yaliyorekodiwa mtandaoni yalihusu kuenea kwa chuki.
Waislamu walidhoofishwa na kulinganishwa na wanyama katika maoni ya mtandaoni, kulingana na ripoti hiyo.
Wengi pia wamewalaumu Waislamu kuwa chanzo cha kueneza chuki dhidi ya Wayahudi, ripoti ilisema.
Ripoti ilisema 40.8% ya kesi zote zilizoripotiwa ni kuhusu ukosefu wa usawa na 19.5% zilihusisha matusi. Kesi za kuenea kwa chuki zilikuwa 8.9% na 2.6% ilihusisha mashambulizi ya kimwili.
Kesi zilizobakia zilikuwa ni za uharibifu (7.5%), vurugu za polisi (7.3%), vitisho hatari (3.2%), uchochezi wa chuki (1.8%), uonevu na kuvizia (0.8%) na kesi nyenginezo (7.7%).
Katika ripoti yake, kituo hicho cha nyaraka kilisisitiza kwamba takwimu zake ni muhtasari na kwamba idadi halisi ya kesi inadhaniwa kuwa kubwa zaidi.
Shirika hilo limesema takwimu hizo zinaleta wasiwasi na kuzidi kuchangia mgawanyiko katika jamii. Kituo cha uhifadhi wa nyaraka, kwa hivyo, kimetoa wito wa kupewa mbele zaidi kesi za chuki dhidi ya Uislamu.