‘Pele’ sasa ni neno linalomuelezea ‘mchezaji wa kipekee’ baada ya jina la bingwa huyo wa mara tatu wa kombe la dunia kama neno jipya katika kamusi ya kireno ijulikanayo kama Michaelis Dictionary.
“Pele” ambaye jina lake halisi ni Edson Arantes do Nascimento, ndiye mchezji bora zaidi duniani wa soka.
Mapema mwezi huu taasisi ya kumuenzi Pele, ilizindua kampeni ya “Pele katika Kamusi” ili kumpa sifa na kutambua umuhimu wake katika Nyanja zingine mbali na michezo.
Siku ya Jumatano, neno “Pele” lilijumuishwa pamoja na zaidi ya maneno mengine 167,000 katika kamusi ya Michaeli, inayochapishwa nchini Brazil kwa lugha ya Kireno.
Wazungumzaji zaidi ya milioni 265 wa lugha ya Kireno kote duniani, sasa wanaweza kutumia neno ‘Pele’ kumaanisha mtu aliye na kipaji cha kipekee, ambapo tayari inatumika hivyo nchini Brazil kwa utani.
“Neno ambalo tayari lilikuwa linatumika kiutani sasa limewekwa katika kumbukumbu ya milele katika kamusi ya Brazil!” Ilichapisha taasisi ya wakfu wa Pele katika mtandao wa Instagram.
Katika chapisho lipya, neon hilo limeelezewa kama “mtu wa ajabu, asiye na mfano,tofauti kabisa” maelezo ambayo yamehusishwa sana na ‘Mflame’ wa soka, ambaye alifariki Disemba 2022 akiwa na miaka 82.
Ukurasa wa mtandao wa Kamusi hiyo pia umetoa mfano wa utumiaji wa neno hilo kama: ‘ Huyu ndiye Pele wa mpira wa vikapu.’ Au ‘ Huyu ndiye Pele wa uigizaji Brazil’
Kwa sasa neno hilo limo katika kamusi ya Michaeli tu, japo kuna mipango ya kuliingiza katika kamusi zingine zilizo chapishwa duniani.