Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ametoa wito kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kukomesha vita vya Israeli huko Gaza, akisema kuwa Israeli ilikuwa karibu kabisa kuangamiza na imekaribia kutofaa tena watu kuishi.
Abbas ameongeza kuwa Israeli, ambayo imekuwa ikikataa kutekeleza maazimio ya Umoja wa Mataifa haistahili kuwa mwanachama wa Shirika hilo.
"Wazimu huu hauwezi kuendelea. Ulimwengu wote unawajibika kwa kile kinachotokea kwa watu wetu," aliuambia Mkutano Mkuu wa wanachama 193.
Vita vya Israeli dhidi ya Gaza, ambavyo sasa vimeingia siku yake ya 356, vimewaua Wapalestina wasiopungua 41,534.
Isitoshe, zaidi ya watu 620 wameuawa tangu Septemba 23 katika shambulio kubwa la mabomu la Israeli nchini Lebanon.
TRT World