Vita vya Israeli dhidi ya Gaza iliyozingirwa vilivyoingia siku ya 84 vimesababisha vifo vya Wapalestina 21,507. / Picha: AA

Takriban Wapalestina 187 wameuawa kwenye mashambulizi ya Israel Gaza ndani ya saa 24 iliyopita, na kufikisha idadi ya vifo 21,507 tangu Oktoba 7, hayo ni kwa mujibu wa Wizara ya Afya katika Gaza.

Wizara hiyo pia imeongeza kuwa watu 55,915 wamejeruhiwa tangu kuanza kwa vita vya Israeli kwenye eneo hilo.

Kulingana na Umoja wa Mataifa zaidi ya asilimia 80 ya watu milioni 2.4 wa Gaza wamefurushwa makwao, tangu vita vya kikatili vya Israeli dhidi ya Gaza vilipoanza Oktoba 7.

Israel yawazuia wapalestina kuingia Msikiti wa Al Aqsa Ijumaa ya 12 mfululizo

Mamlaka ya Israel imewazuia Wapalestina kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa katika eneo la Jerusalem Mashariki, hii ikiwa ni Ijumaa ya 12 mfululizo.

Idadi kubwa ya maafisa wa Polisi wa Israel walitawanywa katika eneo hilo kuzuia waumini kuingia msikitini, mashahidi waliiambia Anadolu.

Watu walioshuhudia waliongeza kusema kuwa polisi wa Israeli waliweka vizuizi kwenye milango ya mji wa zamani na kuruhusu wazee tu kuingia msikiti huo wa Al Aqsa.

Madaktari wasio na mipaka MSF wasisitiza usitishwaji wa mapigano mara moja Gaza

Shirika la Madaktari wasio na Mipaka (MSF) wamesisitiza haja ya kusitisha mapigano huko Gaza mara moja.

"Kushindwa kwa Marekani kuidhinisha mfululizo wa maazimio ya UN yanayotoa wito wa kusitisha mapigano Gaza kumesababisha kupitishwa kwa azimio llilopunguzwa nguvu ambalo halina maana kwetu," Jacob Burns, mratibu wa mradi wa MSF huko Gaza, alisema katika taarifa.

"Vizuizi vya kuleta misaada kupitia njia ngumu ya vituo vya ukaguzi vya Israeli na Misri ni vya kweli, lakini kikwazo kikuu kwa wahudumu wetu wa matibabu wanaojaribu kutoa huduma zaidi na bora ya afya hapa ni kuendelea kwa vurugu," ilisema taarifa hiyo.

TRT World