Waziri wa urithi wa israel, Amichay Eliyahu Picha : TRT

Waziri wa urithi wa israel Amichai Eliyahu amesema kuwa kuangusha "bomu la nyuklia" katika eneo la Gaza ni "chaguo", kulingana na vyombo vya habari vya Eneo hilo.

Eliyahu, Waziri wa Chama cha kulia cha Otzma Yehudit, alisema kuwa "moja ya uwezekano wa Israeli katika vita huko Gaza ni kutupa bomu la nyuklia kwenye ukanda huo", gazeti la Daily Times ya Israeli iliripoti.

Akizungumza katika mahojiano ya redio, Eliyahu pia " amepinga vikali kuruhusu misaada yoyote ya kibinadamu kuingia Gaza.”

"Hatutatoa misaada ya kibinadamu kwa Wanazi", Waziri huyo alisema, akiongeza kuwa " hakuna kitu kama raia wasiohusika huko Gaza.”

Waziri huyo wa mrengo wa kihafidhina pia alisema kuwa watu wa Palestina "wanaweza kwenda Ireland au jangwa, majitu hao wa Gaza wanapaswa kujitafutia suluhisho peke yao.”

Aliongeza kuwa "Mtu yeyote anayepeperusha bendera ya Palestina au Hamas hapaswi kuendelea kuishi kwenye uso wa dunia".

'Wenye msimamo mkali serikalini'

Wakati huo huo, kiongozi wa upinzani Yair Lapid aliomba Eliyahu aachishwe kazi kwa sababu ya matamshi yake.

Lapid alisema matamshi hayo ni " yenye kushtua na ya kichaa ya mhudumu asiye na cheo.”

"Aliathiri familia za watekaji nyara, aliumiza jamii ya Israeli na kudhuru msimamo wetu wa kimataifa," alisema kupitia jukwaa la mtandao wa kijamii, X.

"Uwepo wa watu wenye itikadi kali serikalini unatuhatarisha sisi na mafanikio ya malengo ya vita - kuishinda Hamas na kuwarudisha wote waliotekwa nyara," kiongozi huyo wa upinzani ameongeza.

Pia alisisitiza Kuwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu " lazima amfukuze kazi asubuhi ya leo.”

Baada ya saa moja kufuatia taarifa hiyo, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alimsimamisha kazi waziri wa urithi kutoka mikutano ya serikali kwa muda usiojulikana, ofisi ya waziri mkuu ilisema.

TRT World