Shirika la Umoja wa Mataifa limesema watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyolenga kituo cha UN mjini Gaza, ambapo mamia ya Wapalestina walikimbilia kutafuta hifadhi wakitoroka vita.
"Shambulio hilo limeripotiwa kusababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi," idhaa ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa ilisema katika taarifa iliyotolewa mwishoni mwa Jumamosi.
Israel imekuwa ikipiga mabomu yaliyolenga Ukanda wa Gaza tangu wapiganaji wa Hamas walipofanya shambulio la dhidi ya jamii za kusini mwa Israeli mnamo Oktoba 7.
"Msiba unaoendelea wa vifo na majeraha kwa raia walionaswa katika mzozo huu haukubaliki na lazima usitishwe." taarifa ya UN ilisema.
Wizara ya Afya ya Gaza haijatoa takwimu mpya za majeruhi kwa saa 48, ikisema kuwa haijaweza kufanikisha mawasiliano na hospitali.
Wizara hiyo iliongeza kuwa miili kadhaa imetawanyika mitaani huku ambulansi zikishindwa kuwafikia majeruhi kutokana na mapigano makali na mabomu.