Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa /Picha: AFP

Afrika Kusini imeitaka Jumuiya ya Kimataifa, wakiwemo washirika wa Israeli, kutokufumbia macho mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina, yanayoendelea katika ukanda wa Gaza.

"Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na Israeli umeongeza umefikia viwango visivyoeleweka vya ukatili, chuki na ukandamizaji wa kikatili uliokithiri.

Dunia lazima ifanye ziada kumaliza mateso ya Wapalestina, hususani ya wanawake na watoto wengi wasio na hatia,” amesema Rais Cyril Ramaphosa katika taarifa.

Eneo la Rafah, linalopatikana kusini mwa ukanda wa Gaza, lina jumla ya wapalestina milioni 1.5, waliokimbia machafuko ya huko Gaza.

Mwishoni mwa mwaka jana, Afrika Kusini iliishitaki Israeli kwenye Mahakama hiyo kubwa ndani ya Umoja wa Mataifa, ambapo inatuhumiwa kwa mauaji ya kimbari.

Mnamo Januari, uamuzi wa muda ulisema "inawezekana" kwamba Tel Aviv inafanya mauaji ya halaiki katika eneo la pwani, na kuamuru Tel Aviv kusitisha vitendo kama hivyo na kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa raia wanapokea msaada wa kibinadamu.

Kiongozi huyo wa Afrika Kusini alisema maombi yao ya hivi karibuni ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki, yanafuatia kuongezeka kwa Israel kwa mashambulizi yake dhidi ya Rafah, ambayo yamezidisha hali mbaya na kusababisha madhara makubwa.

Afrika Kusini ilisema hatua za awali za muda zilizowekwa na Mahakama hiyo kuhusu Israel hazitekelezwi, na kwamba hali imebadilika sana tangu amri ya mwisho ya mahakama hiyo Machi 28.

Ramaphosa alisema nchi yake inaendelea kuamini kwamba usitishaji vita wa kudumu huko Gaza unahitajika ili hatua za muda za mahakama zitekelezwe ipasavyo.

Aliongeza kuwa nchi yake inatiwa moyo sana na maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Marekani na sehemu nyingine za dunia.

"Pia tumetiwa moyo sana na kupitishwa kwa rasimu ya azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambalo linapendekeza kwa Baraza la Usalama kufikiria upya ombi la Taifa la Palestina kwa uanachama kamili wa Umoja wa Mataifa," alisema.

TRT Afrika