Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewajulisha maofisa wa Israeli umuhimu wa kusitisha mashambulizi zaidi dhidi ya Lebanon na Hezbollah.
Blinken alikutana mshauri wa usalama wa Israeli Tzachi Hanegbi na Waziri wa Masuala ya Kimkakati Ron Dermer, imesema ofisi ya Mambo ya Nje katika taarifa yake.
Akisisitizia "dhamira ya dhati" ya Marekani kwa usalama wa Israel, Blinken alijadili juhudi zinazoendelea za kufikia usitishaji vita huko Gaza na kuhakikisha kuwa mateka wote wanaachiwa.
"Waziri alisisitiza haja ya juhudi za ziada za kuongeza misaada ya kibinadamu katika eneo la Gaza na ujenzi mpya wa eneo hilo," taarifa hiyo iliongeza.
Mkutano huo umekuja baada ya jeshi la Israel kusema kuwa limeidhinisha mipango ya operesheni ya mashambulizi dhidi ya kundi la Hezbollah la Lebanon ambalo limetuma ndege zisizo na rubani nchini Israel katika kipindi cha miezi minane iliyopita, huku kikishambuliana kwa mabavu na wanajeshi wa Israeli.