Mexico imeikabidhi Marekani Ovidio Guzmán López, mwanawe  "El Chapo"/ Picha: AFP

Ovidio Guzman Lopez, kwa jina maarufu "El Raton" au "Panya," alishtakiwa mapema mwaka huu kwa madai ya ulanguzi wa dawa za kulevya unaohusuina na kashfa la fentanyl linaolikabili Marekani.

Baba yake "El Chapo" alihukumiwa mnamo 2019 kwa kuendesha kile kilichoaminika kuwa kikundi kikubwa zaidi cha dawa za kulevya duniani na anatumikia kifungo cha maisha katika gereza la supermax, Colorado, Marekani.

Garland aliisifu usafirishaji huo kama " hatua ya hivi karibuni kwenye juhudi za Idara ya sheria kushambulia kila nyanja ya shughuli za walanguzi hao.

El Chapo. Picha: AP

"Wizara ya sheria itaendelea kuwawajibisha wale wote wanaohusika na uchochezi wa janga la 'opioid' ambalo limeharibu jamii nyingi kote nchini."

Ikulu ya Marekani White House pia imesifu uhamisho huo kama mojawapo ya" ushirikiano wa karibu unaoendelea " na Mexico, ishara kuwa utawala wa Rais Joe Biden una hamu ya kuvuka msuguano na Mexico juu ya juhudi za kupambana na dawa za kulevya.

"Tunawashukuru wenzetu Mexico kwa ushirikiano wao kwenye juhudi za kuwalinda watu wetu dhidi ya wahalifu jeuri," ilisema taarifa ya Mshauri wa Usalama wa Ndani Liz Sherwood-Randall, iliyotolewa na Ikulu ya white House.

Mwanasheria Mkuu Wa Marekani Merrick Garland. Picha: Reuters

Ushirikiano kati ya vikosi vya Usalama vya Mexico na Marekani ulipungua mwaka jana baada ya Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador kubandua kitengo kilichokuwa kikifanya kazi kwa karibu na mawakala wa mamlaka ya Marekani inayokabiliana na Dawa za Kulevya kwa zaidi ya miaka 25.

Kiongozi huyo wa Mexico aliwashutumu mawakala wa Marekani kwa "kuingilia mambo ya nchi yake".

"Chapos mchanga'

Baada ya "El Chapo" kuhukumiwa, wanae kadhaa, wanaojulikana kwa pamoja kama "Chapos changa", walirithi udhibiti wa genge la Sinaloa, mamlaka ya Marekani ilisema.

Maofisa wa usalama walimkamata "El Chapo mchanga" katika mji wa Sinaloa wa Culiacan mnamo Januari 5.

Emma Coronel, mkewe El Chapo anayeshikilia uraia wa Marekani, ameachiliwa huru. Picha AFP

Operesheni ya kumkamata "El Chapo mchanga" ilisababisha vifo 29, ikiwa ni pamoja na wanajeshi 10 na wahalifu walioshukiwa 19 katika mapigano na ghasia wakati wanachama wa genge walipojaribu kumwachilia huru.

Washiriki wa genge waliteketeza magari, huku sauti ya mapigano makubwa ya risasi yakiskika mnamo 2019 wakati "El Chapo mchanga" aliposhikiliwa kwa muda mfupi kabla ya kuachiliwa ili kuepuka umwagaji damu.

Wakati huo, mamlaka ya Marekani iliweka zawadi ya dola milioni 5 kwa kukamatwa kwake, huku ikimshtaki yeye na ndugu yake, Joaquin Guzman Lopez, kwa kusimamia maabara ya methamphetamine katika jimbo la Sinaloa ikizalisha takriban kilo 2,000 hadi 4,000 za meth kwa mwezi.

Mwanachama wa genge la Sinaloa akiandaa vidonge vya dawa ya kulevya aina ya methamphetamine, Mexico. Picha: Reuters

"Taarifa zingine zinaonyesha kuwa Ovidio Guzman Lopez aliamuru mauaji ya majasusi, mlanguzi wa dawa za kulevya, na mwimbaji maarufu wa Mexico ambaye alikataa kuimba kwenye harusi yake", kulingana na tovuti ya Uhamiaji wa Marekani.

Coronel, anayeshikilia uraia wa Marekani na Mexico, licha ya kutokuwa mama mzazi wa Guzman, aliachiliwa huru kutoka Nyumba moja mjini California wiki hii baada ya kumaliza hukumu kwa kushirikiana na Chapo Guzman katika shughuli zake za mihadarati.

AFP