Maandamano ya vyuo vikuu ya kuunga Mkono Palestina yamekuwa yakiendelea tangu Aprili 17 / Picha: AA

Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu cha Columbia mjini New York, Marekani, aliharibu cheti chake wakati wa mahafali ili kupinga madai ya taasisi ya elimu ya kuhusika katika "mauaji ya kimbari" ya Israeli dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Tarsis Salome, mhitimu wa kazi ya kijamii kutoka chuo hicho cha Columbia, akiwa amevaa keffiyeh na mikono iliyofungwa, alirarua cheti chake vipande vipande alipokuwa jukwaani kwenye sherehe ya kuanza siku ya Ijumaa.

Hatua hiyo imejiri baada ya chuo hicho kikuu kuondoa hafla kuu ya kuhitimu kutokana na hofu kuu ya usalama baada ya baadhi ya wanafunzi wanaounga mkono Palestina kukita kambi katika eneo hilo.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Columbia walionekana wakiwa wamevaa pingu na kuonyesha ishara na bendera za Wapalestina wakati wa sherehe.

Zaidi ya watu 2,000 wamekamatwa katika vyuo vikuu nchini Marekani tangu mwezi uliopita huku kukiwa na mijadala mikali kuhusu haki ya kuandamana, mipaka ya uhuru wa kujieleza na tuhuma za chuki dhidi ya wayahudi.

Maandamano na mshikamao wa kuketi pia yanafanyika katika vyuo vikuu katika sehemu za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Uholanzi na Uswisi.

Maandamano ya vyuo vikuu ya kuunga Mkono Palestina yamekuwa yakiendelea tangu Aprili 17, wakati wanafunzi wa Chuo kikuu cha Columbia walipoanzisha kambi kuonyesha mshikamano na Gaza na kudai shule yao ijitenge na Israeli.

AA