Kulingana na mashuhuda, mabomu hayo yalilenga vikundi vya raia, waandishi wa habari na mahema ya watu wasio na makazi./Picha: Reuters             

Takribani Wapalestina 17, wakiwemo waandishi wa habari, wameuwawa na majeshi ya Israeli katika maeneo tofauti ya eneo la Gaza.

Timu za madaktari zililiambia shirika la habari la Anadolu kuwa Wapalestina 13 waliuwawa kufuatia shambulio la bomu katika eneo la al-Shakoush, lililoko kaskazini mwa Rafah, kusini mwa Gaza.

Kulingana na mashuhuda, mashambulizi hayo yaliwalenga waandishi wa habari, raia wa kawaida wa watu waliokosa makazi.

Duru za kiafya pia zimesema kuwa Wapalestina wanne waliuwawa na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulio la bomu lililolenga makazi ya familia ya Al Ghazi katika kitongoji cha Sabra, kusini kwa mji wa Gaza.

Wakati huo huo, mashuhuda wanasema kuwa vifaru na matingatinga ya kijeshi yaliharibu eka 1,235 za mazao ya mbogamboga, kaskazini mwa Rafah, eneo pekee lililotengwa kwa shughuli hiyo.

TRT Afrika