Familia za Wapalestina zimewakaribisha watoto 30 na wanawake 3 walioachiliwa kutoka jela za Israel kama sehemu ya makubaliano ya mapatano na kundi la upinzani la Hamas. Hii inafikisha 150 Wapalestina walioachiliwa.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yamerefushwa kwa siku mbili zaidi, na ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imesema imeidhinisha wanawake 50 zaidi wa Kipalestina katika orodha yake ya kutolewa.
Familia za Wapalestina zilikumbatiana kwa furaha wapendwa wao walioachiliwa. Hapa ni baadhi ya matukio kwa picha:
Mpalestina Muhammad Abu Al-Humus akimkumbatia mama yake aliporejea nyumbani kwake katika Jerusalem Mashariki inayokaliwa kwa mabavu.
Mtoto wa Kipalestina akimkumbatia mama yake baada ya kuachiliwa kutoka jela ya Israel badala ya mateka wa Israel walioachiliwa na Hamas kutoka Gaza iliyozingirwa, huko Ramallah katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Mpalestina akijibu baada ya kuachiliwa kutoka jela ya Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.
Mpalestina aliyeachiliwa huru aonyesha hisia ya furaha baada ya kutoka katika jela ya kijeshi ya Israel, Ofer.
Mpalestina afurahia baada ya kuachiliwa kutoka jela ya Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.
Mpalestina [aliyevaa jumper ya kijivu] akiashiria wafuasi na jamaa baada ya kuachiliwa kutoka jela ya Israeli.
Mwanamke wa Kipalestina aliyeachiwa huru akifurahia baada ya kuondoka katika jela ya kijeshi ya Israel, Ofer, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.