Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus, ana matumaini kuwa Marekani itafikiria upya uamuzi wake kujiondoa kutoka shirika hilo./Picha: Reuters            

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa ana matumaini kuwa Marekani itafikiria upya uamuzi wake wa kutaka kujiondoa kwenye shirika hilo.

Mara baada ya uapisho wake, Trump alitia saini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa WHO.

" Marekani ilikuwa mwanachama mwanzilishi wa WHO mwaka wa 1948 na imeshiriki katika kuunda na kusimamia kazi ya WHO tangu wakati huo, pamoja na Mataifa mengine Wanachama 193, ikiwa ni pamoja na kupitia ushiriki wake katika Baraza la Afya Ulimwenguni na Bodi ya Utendaji," alisema Adhanom katika taarifa yake.

Hata hivyo, Trump ameitupia lawama WHO kwa kushindwa kupitisha mageuzi ya haraka, akiongeza kuwa shirika hilo lilishindwa kushughulikia janga la Uviko 19 ipasavyo.

"WHO inaendelea kudai malipo isivyo halali kutoka kwa Marekani enye kutaabisha isivyo haki kutoka Marekani, mbali na uwiano na malipo yaliyotathminiwa ya nchi nyingine. China, yenye idadi ya watu bilioni 1.4, ina asilimia 300 ya wakazi wa Marekani, lakini inachangia karibu chini ya asilimia 90 ya WHO," imesema.

WHO inaitambua Marekani kuwa na mchango na ufadhili mkubwa kwa kwazi yake.

" Marekani ndiye mfadhili mkuu na mshirika wa WHO, ikichangia kupitia michango na ufadhili wa hiari. Marekani ilichangia dola za Marekani zaidi ya bilioni 1.28 wakati wa miaka miwili ya 2022-2023," WHO imesema katika tovuti yake.

Rais Trump amebatilisha barua ya Rais kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyotiwa saini Januari 20, 2021, ambayo ilibatilisha ombi la Marekani la Julai 6, 2020.

" Tunatumai Marekani itafikiria upya na tunatazamia kushiriki katika mazungumzo yenye kujenga ili kudumisha ushirikiano kati ya Marekani na WHO, kwa manufaa ya afya na ustawi wa mamilioni ya watu duniani kote," Adhanom ameongezea.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT Afrika