Idadi ya vifo vya Wapalestina huko Gaza imefikia 3,300 kutokana na mashambulizi yanayoendelea ya Israel huko Gaza tangu Oktoba 7, waziri wa afya wa Palestina amesema.
"Idadi ya mashahidi katika Gaza inazidi Wapalestina 3,300, wakati idadi ya waliojeruhiwa ni zaidi ya 13,000," Waziri wa Afya Mai al Kaila alisema katika mkutano na waandishi wa habari huko Ramallah, na kuongeza kuwa idadi hiyo inakadiriwa kutokana na hali mbaya ya Gaza kama matokeo ya kuendelea kwa mashambulizi ya Israel.
Pia alisisitiza kuwa, kuna uhaba mkubwa wa madawa huko Gaza, pamoja na matatizo ya watu kupata hospitali.
Kukatwa kwa huduma ya maji kumeongeza hatari za kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza.
Kundi la Palestina la Islamic Jihad limekanusha mashambulizi
Kundi la Palestina la Islamic Jihad limekanusha madai ya Israel kwamba iliishambulia hospitali ya Al Ahli Arab huko Gaza siku ya Jumanne kwa roketi ambayo haikurushwa kimakosa na kusababisha vifo vya mamia ya watu.
Kundi hilo katika taarifa yake siku ya Jumatano lilisema kuwa majaribio ya Israel ya kuinyooshea vidole hayana msingi, na kusisitiza kwamba haitumii vituo vya umma, haswa hospitali, kwa madhumuni ya kijeshi.
Taarifa hiyo ilisema kuwa vuguvugu hiyo, pamoja na vikundi vyengine vya upinzani huko Gaza, "Limejitolea kutotumia maeneo ya ibada, vituo vya umma, haswa hospitali, vituo vya kijeshi, au kuhifadhi silaha," na inachukulia "shutuma za Israeli kama jaribio kubwa la kukwepa kuwajibika kwa uhalifu kama huo na kulenga hospitali zingine".
China yahimiza kusitishwa kwa mapigano
China siku ya Jumatano ililaani vikali shambulio la Israel dhidi ya hospitali ya Baptist ya Al-Ahli katikati mwa Gaza, ikisema "imeshtushwa" na tukio hilo.
"Tunaomboleza kwa ajili ya waathirika na tunatoa pole kwa waliojeruhiwa," ilisema taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje kufuatia shambulio la Jumanne usiku ambalo lilisababisha vifo vya mamia. Ikitoa wito wa "kusitishwa mara moja kwa mapigano na kukomesha uhasama," Beijing ilihimiza.
"Kila jitihada zinazowezekana za kulinda raia na kuepusha maafa mabaya zaidi ya kibinadamu," Chian imesema.
Putin: Shambulizi la Hospitali ya Gaza ni 'tukio baya
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameelezea shambulio dhidi ya hospitali ya Baptist ya Al-Ahli katikati mwa Gaza na kuua mamia ya watu kuwa ni "tukio baya na janga."
"Kuhusu shambulio la hospitali, mkasa uliotokea pale, ni tukio baya sana, mamia ya waliofariki, mamia ya waliojeruhiwa. Hili bila shaka ni janga," Putin aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Beijing, ambapo yupo kuhudhuria kongamano la tatu la Belt and Road.
Kiongozi wa Urusi alisema anatarajia kuwa tukio hilo litakuwa ishara ya kumaliza mzozo huu haraka iwezekanavyo, na kuanza "baadhi ya mawasiliano na mazungumzo."
Papa Francis asikitishwa na hali ya "kukata tamaa" huko Gaza
Kiongozi wa kanisa katoliki, Papa Francis alisikitishwa na hali ya "kukata tamaa" huko Gaza siku ya Jumatano huku akiwahimiza waumini kuchukua "upande mmoja tu" katika mzozo wa Israel na Hamas, yaani "upande wa amani."
Akizungumza wakati wa hadhira yake ya kila wiki katika Uwanja wa St Peter's Square, Papa alisema,
"Vita havisuluhishi tatizo lolote, vinaongeza tu kifo na uharibifu, huongeza chuki, huzidisha kisasi. Vita hufuta siku zijazo," alisema.
Aliomba juhudi zote zinazowezekana "kuepusha janga la kibinadamu," na akatangaza maombi maalum ya amani katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mnamo Oktoba 27, ambayo wale wote wanaojali amani ya dunia wanaalikwa kujumuika nayo.
siku ya Jumatano huku akiwahimiza waumini kuchukua "upande mmoja tu" katika mzozo wa Israel na Hamas, upande wa "amani." Akizungumza wakati wa hadhira yake ya kila wiki katika Uwanja wa St Peter's Square, Papa alisema: "Vita havisuluhishi tatizo lolote, vinapanda tu kifo na uharibifu, huongeza chuki, huzidisha kisasi. Vita hufuta siku zijazo". Aliomba juhudi zote zinazowezekana "kuepusha janga la kibinadamu", na akatangaza maombi maalum ya amani katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mnamo Oktoba 27, ambayo wale wote wanaojali amani ya dunia wanaalikwa kujumuika nayo.