Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) amehimiza kufiksishwa haraka kwa misaada ya kibinadamu huko Gaza, Palestina, huku kukiwa na ripoti za vifo vinavyohusiana na homa ya baridi kali ya watoto waliozaliwa hivi karibuni na watoto wachanga.
"Ripoti za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa za watoto wanaokufa kutokana na homa ya baridi kali huko Gaza zinasisitiza ukali mkubwa wa mgogoro wa kibinadamu huko," Jagan Chapagain alisema kwenye mtandao wa X.
"Ninarudia wito wangu wa haraka wa kuruhusiwa wahudumu wa kibinadamu kuingia salama na kutoa msaada wa kuokoa maisha."
"Bila ya watu wa kutoa msaada kuingia salama - watoto wataganda hadi kufa, familia zitakufa njaa na wafanyakazi wa kibinadamu hawawezi kuokoa maisha," Chapagain alisisitiza.
Amesema kwamba ombi lake la dharura kwa pande zote ni kukomesha mateso haya ya kibinadamu sasa.