Jeshi la israel limemkamata mwanaharakati wa upinzani wa Palestina Ahed Tamimi katika mji wa Nabi Saleh ulioko ukingo wa Magharibi, kulingana na mama yake.
"Ahed, 23, alikamatwa katika uvamizi wa nyumba yetu," Nariman Tamimi, alisema Jumatatu.
Aliongeza kuwa majeshi ya Israel yalichunguza nyumba hiyo na kuchukua simu za mkononi za familia hiyo.
"Ahed Tamimi alikamatwa kwa tuhuma za kuchochea vurugu na shughuli za kigaidi katika mji wa Nabi Saleh" karibu na Ramallah, msemaji wa jeshi alisimulia.
"Tamimi alihamishiwa kwa vikosi vya usalama vya Israeli ili kuhojiwa zaidi."
Baba yake Bassem Tamimi alikamatwa na vikosi vya Israel wakati wa uvamizi katika mji huo wiki iliyopita.
'Ishara ya upinzani' mnamo 2017, Tamimi alikamatwa na vikosi vya Israeli baada ya video kuenea ikionyesha msichana huyo, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 16, akiwasukuma na kuwapiga askari wa Israeli ambao walijaribu kuingia nyumbani kwa familia yake.
Baadaye alifungwa kwa kifungo cha miezi minane kwa "kushambulia" askari wa Israeli.
Tangu wakati huo, Tamimi amekuwa ishara ya kimataifa ya upinzani dhidi ya uvamizi wa Israeli Katika Ukingo wa Magharibi.
Kuongezeka kwa ghasia kumesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 150 katika Ukingo wa Magharibi uliokaliwa tangu Oktoba 7, waliouawa na wanajeshi wa Israeli au wavamizi kulingana na Wizara ya Afya ya Palestina.