Hospitali ya Gaza

Akizungumza na mwandishi wa habari wa Reuters, Iyad al-Jaberi, mkurugenzi wa Hospitali ya Aqsa iliyopo eneo la Deir Al-Belah, katikati ya Gaza, aliiambia Reuters kwamba hali katika hospitali hiyo imefikia kiwango cha "hatari."

Imeripotiwa kuwa dawa na vifaa vya tiba vimekwisha katika hospitali ya Aqsa huko Gaza, ambayo imekuwa chini ya kizuizi cha Israeli kwa siku 13.

Jaberi ameongeza, "maelfu ya wamejeruhiwa na maisha ya wagonjwa yako hatarini", huku ikibainika kuwa hospitali hiyo ya Wafia Imani ya Al-Aqsa inatoa huduma kwa maelfu ya wagonjwa katika sehemu ya kati ya Gaza.

"Kwa sababu ya hatua ya Israel ya kufunga njia zote na viingilio vya aina yote vya kuingia na kutoka hadi Gaza tangu tarehe 7 Oktoba, dawa muhimu na vifaa tiba vimeisha katika hospitali hiyo."

Jaberi ametoa wito kwa mashirika ya kimataifa kuingilia kati ili kuishawishi Israeli kuruhusu vifaa tiba kuingia Gaza," alisema.

Nae mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus, katika taarifa yake kuhusu hali ya kiafya ilivyo huko Gaza, jana Jumatano, alibaini kuwa vifaa tiba vilivyotumwa na WHO Gaza vimekwamba mpakani kwa siku ya 4.

Ghebreyesus alisema kuwa upatikanaji wa haraka wa suluhisho unahitajika ili kuanza kupeleka vifaa hivyo vitakavyookoa maisha maisha Gaza, wakati huo huo, akisisisitiza umuhimu wa kukomesha vurugu kati ya pande hizo.

Mgogoro wa Israel na Palestina

Mnamo Oktoba 7, Hamas ilianzisha shambulio kamili dhidi ya Israeli linaloitwa "mafuriko ya Aqsa".

Wakati huo huo, maelfu ya makombora yalipigwa kutoka Gaza kuelekea Israeli, huku makundi yaliyojihami ya Kipalestina yakivamia mpaka wa Beit Hanoun-Erez kwenye mpaka wa Gaza na Israeli na kuuteka.

Vikundi vyenye silaha viliingia katika makazi ya Israeli nalo jeshi la Israeli lilizindua shambulio kwenye Ukanda wa Gaza kwa kutumia ndege kadhaa za kivita.

Hata hivyo, hali hiyo imesababisha Israel kufanya mashambulizi yaliyolenga zaidi raia ambao hayana hatia ikiwemo watoto, wanawake na wazee.

AA